Abiy Ahmed: Bwawa la Renaissance litazifaidisha pia Sudan na Misri
(last modified Mon, 07 Jun 2021 12:52:12 GMT )
Jun 07, 2021 12:52 UTC
  • Abiy Ahmed
    Abiy Ahmed

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa ujenzi wa Bwawa la Renaissance utakuwa na faida si kwa nchi hiyo pekee bali pia kwa nchi za Misri na Ethiopia.

Abiy Ahmed amesema hayo wakati akizindua kiwanda katika eneo la Amhara huko kaskazini mwa Ethiopia na kuongeza kuwa, Bwala la Renaissance litakuwa na faida hata kwa nchi za Misri an Sudan na kwamba, ujenzi wa bwawa hilo unapaswa kukamilishwa kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Ethiopia na nchi nyingine.

Ujenzi wa bwawa hilo ju ya maji ya Mto Nile umezusha mivutano baina ya Ethiopia na nchi za Sudan na Misri.

Misri na Sudan zinasema ujenzi wa bwawa hilo ambalo umegharimu karibu dola bilioni nne, utapunguza maji ya nchi hizo na hivyo kuvuruga maisha ya mamilioni ya watu. Ethiopia nayo inasisitiza kuwa ujenzi wa bwawa hilo ni muhimu kwa ajili ya kueneza umeme katika nchi hiyo ili kuimarisha sekta ya viwanda na pia kuuza bidhaa hiyo katika nchi za nje. Mzozo huo umezusha wasiwasi wa kutokea vita na mapigano baina ya nchi hizo tatu.

Bwawa la Renaissance 

Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri ametishia kwamba "Cairo itatoa jibu lisilotasawarika iwapo nchi yake itapata madhara kutokana na Bwana la Renaissance linalojengwa na Ethiopia juu ya maji ya Mto Nile."

Rais wa Misri alisisitiza kuwa maji ya Misri ni mstari mwekundu na anayetaka kujaribu atakiona cha mtemakuni. 

Ethiopia kwa upande wake imejibu vitisho hivyo ikisema iko tayari kukabiliana na hujuma ya aina yoyote ya adui.

Tags