Waziri Mkuu wa Ethiopia: Hatuna nia ya kujitanua ili kuifikia bahari
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i136706-waziri_mkuu_wa_ethiopia_hatuna_nia_ya_kujitanua_ili_kuifikia_bahari
Waziri Mkuu wa Ethiopia jana alisema kuwa nchi yake "haina nia ya kujitanua" na haina lengo la kuwatishia majirani zake. Amesema vipaumbele muhimu vya kitaifa ni kufikia njia ya baharini na maendeleo ya maji ya Mto Nile.
(last modified 2026-02-17T02:26:18+00:00 )
Feb 17, 2026 02:26 UTC
  • Waziri Mkuu wa Ethiopia: Hatuna nia ya kujitanua ili kuifikia bahari

Waziri Mkuu wa Ethiopia jana alisema kuwa nchi yake "haina nia ya kujitanua" na haina lengo la kuwatishia majirani zake. Amesema vipaumbele muhimu vya kitaifa ni kufikia njia ya baharini na maendeleo ya maji ya Mto Nile.

"Tunaithibitishia dunia nzima kwamba Ethiopia haina malengo ya kijiografia, haina nia ya kujitanua, na haitaki kutishia usalama wa majirani zetu",amesema Abiy Ahmed katika ujumbe wake wa kipekee ulioandikwa kwa lugha ya Kiarabu kabla ya kuanza mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake inafanya juhudi ilikufikia njia ya baharini kama haja muhimu inayotokana na ongezeko la watu na mahitaji ya maendeleo.

Abiy pia amezungumzia mvutano wa kikanda kuhusu maji ya Mto Nile, na kusema jitihada zinazofanywa na Ethiopia kwa ajili maendeleo ya nchi kupitia rasilimali za maji "hazimaanishi kupunguza mgawo wa mtu yeyote wala kukiuka mamlaka ya kujitawala nchi yoyote.Ameutaja Mto Nile kuwa ni tunuya pamoja ambayo inapasa kuwa chachu ya ushirikiano badala ya kuibua migogoro.

Ethiopia imesema kwa muda mrefu kwamba Bwawa lake la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) linalopatikana katika Blue Nile, lenye thamani ya karibu dola bilioni 5 ambalo sasa linafanya kazi ya kuzalisha umeme, ni kitovu cha mkakati wake wa maendeleo na usambazaji wa nishati kwa nchi hiyo yenye zaidi ya watu milioni 120.

Itakumbukwa kuwa nchi zilizo chini ya Mto Nile yaani Misri na Sudan zimekuwa zikibainisha wasiwasi wao kuhusu usalama wa maji kutoka Mto Nile kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nchi hizo.