-
Wapalestina wataka umoja wa kitaifa ili kukabiliana na mpango wa 'Muamala wa Karne'
Jul 07, 2019 07:10Viongozi wa harakati za mapambano ya Palestina wamesisitiza juu ya udharura wa kuweko umoja wa kitaifa huko Palestina ili kukabiliana na mpango uliojaa njama wa Muamala wa Karne.
-
Hamas yaapa kudumaza mpango wa Trump wa "Muamala wa Karne"
Jul 06, 2019 21:54Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa itaendeleza harakati za kupinga mpango eti wa amani uliozusha makelele mengi wa Rais Donald Trump wa Marekani baina ya utawala haramu wa Israel na Wapalestina uliopewa jina la "Muamala wa Karne"
-
HAMAS: Kujiuzulu maafisa wa kijeshi wa Israel ni ishara ya nguvu ya muqawama
Jul 06, 2019 03:45Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, kujiuzulu mkuu wa kitengo cha operesheni cha Shirika la Kiintelijensia la Israel ni jambo linalobainisha juu ya kuchanganyikiwa adui Mzayuni na kuweka wazi nguvu kubwa ya muqawama wa Palestina.
-
Mpango wa Muamala wa Karne, Palestina yakataa upatanishi wa Marekani
Jul 05, 2019 02:36Wiki mbili tu baada ya mkutano wa utangulizi wa kutekeleza mpango uliopewa jina la "Muamala wa Karne" huko Manama nchini Bahrain, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa, Palestina haikubali upatanishi wa Marekani katika kadhia ya Palestina.
-
Abbas apinga upatanishi wa Marekani katika mgogoro wa Palestina
Jul 04, 2019 02:14Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa Palestina haiwezi kukubali upatanishi wa Marekani kati yake na utawala haramu wa Israel.
-
Harakati ya Fat-h yapendekeza kufanyika uchaguzi na kuundwa serikali ya Palestina
Jul 02, 2019 08:07Mshauri wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa Harakati ya Fat-h imetoa pendekezo kwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) la kufanyika uchaguzi na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.
-
Maandamano ya kupinga safari ya Meya wa Israel mjini Paris, Ufaransa
Jul 01, 2019 08:08Wanaharakati na watetezi wa haki za Wapalestina nchini Ufaransa wamefanya maandamano ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris, sambamba na kulaani safari ya Meya wa Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel, nchini humo.
-
Palestina: Kikao cha Manama kinaashiria kufeli utawala wa Trump
Jun 30, 2019 03:38Msemaji wa Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema mkutano wa Marekani uliofanyika siku chache zilizopita katika mji mkuu wa Bahrain, Manama kwa shabaha ya kuzindua Muamala wa Karne umeonesha ni jinsi gani sera na mipango batili ya utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani imefeli.
-
Kamati ya Mshikamano wa Wakenya na Wapalestina: Muamala ya Karne utagonga mwamba
Jun 27, 2019 12:29Vuguvugu la mshikamano baina ya Wakenya na Wapelestina limekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
PLO: Marekani inakusudia kubuni mipaka mipya eneo la Asia Magharibi
Jun 27, 2019 03:25Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO, amesema kuwa mkutano wa kiuchumi wa mjini Manama, Bahrain umefeli kufikia malengo yake na kuongeza kuwa Marekani inakusudia kubuni mipaka mipya katika eneo la Asia Magharibi na kuanzisha muungano ulio dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.