Mufti wa Syria: Waislamu waungane katika suala la Palestina
Mufti Mkuu wa Syria amewahimiza Waislamu washikamane na kuwa kitu kimoja dhidi ya njama zinazopikwa na maadui dhidi ya kadhia ya Palestina.
Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun ametoa wito huo katika mazungumzo yake na mshauri wa Rais Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Muhammad al Hayash mjini Damascus na kusisitiza kuwa: Suala la Palestina linapewa kipaumbele nchini Syria na kwamba mashinikizo yote yanayofanywa dhidi ya nchi hiyo yanatokana na misimamo imara ya serikali ya Damascus kuhusu kadhia ya Plestina.
Sheikh Badreddin Hassoun ametilia mkazo nafasi na mchango wa wanazuoni na maulama wa Kiislamu kwa ajili ya kukabiliana na fikra za kuchupa mipaka na kupambana na wimbi linalochafua sura safi ya Uislamu.
Kwa upande wake, mshauri wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amewahimiza wanazuoni wa Kiislamu kuunganisha pamoja safu za Umma wa Kiislamu na kuwakutanisha pamoja katika kutetea kadhia yao muhimu zaidi ambayo ni suala la Palestina.