-
Jeshi la Israel laendeleza ukatili wake, laua Wapalestina 7 Gaza
Sep 29, 2018 04:43Kwa akali Wapalestina saba wameuawa shahidi huku wengine zaidi ya 500 wakijeruhiwa baada ya jeshi la Israel kuwamiminia risasi na kuvurumishia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Ziyad Al-Nakhalah achaguliwa Katibu Mkuu mpya wa Jihadul-Islami ya Palestina
Sep 28, 2018 23:15Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imetangaza kuwa katika uchaguzi wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo, Ziyad Al-Nakhalah amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Dakta Ramadhan Abdullah Shalah.
-
Stratijia ya Wapalestina kwa ajili ya kukabiliana na "Muamala wa Karne"
Sep 27, 2018 22:52Vyama na makundi ya mapambano ya ukombozi wa Palestina Jumatano iliyopita yaliandika na kutayarisha mpango wa "Uokovu wa Taifa" kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichopewa jina la "Muamala wa Karne" uliotayarishwa na Marekani kwa shabaha ya kumaliza kabisa kadhia ya Palestina.
-
Afrika Kusini yakanusha taarifa za kurejea tena balozi wake mjini Tel Aviv
Sep 26, 2018 23:30Serikali ya Afrika Kusini imekanusha taarifa zilizoenea kwamba, imemrejesha huko Tel Aviv balozi wake ambaye ilimwita nyumbani mwezi Mei mwaka huu.
-
Ismail Hania ataka kuhitimishwa masaibu na machungu ya taifa la Palestina
Sep 26, 2018 23:29Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameyataka mataifa ya dunia, kufanya hima kwa ajili ya kuhitimisha masaibu na machungu wanayokabiliwa nayo wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Utawala wa Kizayuni watoa muhula wa mwisho kwa wakazi wa kijiji cha Khan al Ahmar; wawataka waondoke kijijini hapo
Sep 23, 2018 23:28Utawala wa Kizayuni umewapa wakazi wa kijiji cha Khan al Ahmar katika mji wa Quds muda wa siku saba wawe wameondoka kijijini hapo.
-
Hamas: Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kikwazo katika kuboreka hali ya mambo Ghaza
Sep 23, 2018 10:32Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kikwazo kikuu katika kuboreka hali ya mambo ya Ukanda wa Ghaza.
-
HAMAS: Matamshi ya Mahmoud Abbas yanabainisha mtazamo wake binafsi
Sep 22, 2018 13:14Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuhusu matamshi aliyotoa Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kuwa tayari kufanya mazungumzo na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, kwamba matamshi hayo yanaakisi mtazamo wake binafsi, wala hayawakilishi maoni ya wananchi wa Palestina.
-
Udharura wa kulazimishwa Israel kujiunga na mkataba wa nyuklia wa NPT
Sep 22, 2018 03:58Katika Mkutano Mkuu la 62 la Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, kumesisitiziwa wajibu na udharura wa kulazimishwa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kujiunga na Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia, NPT.
-
Saudia yawapiga marufuku Wapalestina laki 6 kwenda kuhiji
Sep 21, 2018 09:10Utawala wa Aal-Saud umewapiga marufuku Wapalestina laki sita kwenda katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kushiriki ibada za Hija na Umra.