Wazayuni waendelea kuiba viungo vya miili ya watoto Wapalestina
Kwa mara nyingine tena utawala haramu wa Israel umetuhumiwa kuiba viungo vya miili ya watoto wa Kipalestina.
Tovuti ya De Wereld Morgen imekataa ombi la shirika la Interfederal Center for Equal Opportunities la Ubelgiji lililoitaka ifute makala iliyoichapisha kuhusu jinai hiyo ya Wazayuni dhidi ya watoto wa Kipalestina.
Makala hiyo iliyoandikwa na Robrecht Vanderbeeken, katibu wa masuala ya utamaduni wa muungano wa kibiashara wa ACOD nchini Ubelgiji ilifichua kuwa, kizazi cha Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kinaendelea kuangamizwa kwa njaa na sumu, huku watoto wa Kipalestina katika ukanda huo wakitekwa nyara, kuuawa na kisha viungo vyao kunyofolewa.
Hii si mara ya kwanza utawala haramu wa Israel kutuhumiwa kwamba unaiba viungo vya miili ya Wapalestina.
Mkutano uliofanyika nchini Ujerumani mwaka 2016 kujadili hali ya kijamii ya vijana wa Palestina ulilituhumu jeshi la Israel kuwa linaiba viungo vya raia wa Palestina na kufanya mauaji ya kimbari huko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.
Novemba mwaka 2015, Riyad Mansour, Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa alimuandikia barua Katibu Mkuu wa umoja huo, akimtaarifu kuwa, miili ya watoto wa Kipalestina waliotekwa nyara na kuuawa na jeshi katili la Israel imenyofolewa baadhi ya viungo, kama vile konea za macho.
Kabla ya hapo, Kituo cha Utafiti cha Jerusalem kiliripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeiba viungo vya Wapalestina 138 waliouawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa Israel.