WHO yaonya kuwa Uganda ingali iko katika hatari ya mripuko wa ebola
Shirika la Afya Duniani, WHO leo limetoa indhari kwa Uganda kwamba ingali iko katika hatari kutokana na mripuko wa ugonjwa wa Ebola ulioenea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
WHO imetoa tahadhari hiyo baada ya nchi hiyo kufurahia kumalizika kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika taifa hilo.
Uganda ilikamilisha siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho aliyekuwa ameambukizwa kuruhusiwa kutoka hospitali Juni 16, na tangu wakati huo hakujakuwa na maambukizi yoyote yaliyothibitishwa.
Siku ya Jumanne, wizara ya afya ya nchi hiyo ilisema "imefarijika kutangaza rasmi kuwa Uganda haina tena maambukizi ya mripuko wa ugonjwa wa Ebola 2026 ikiongeza: "Sasa hivi, hakuna tena Ebola Uganda."
Lakini Shirika la Afya Duniani limesema utaratibu wa kimataifa ni kuwa siku 42 baada ya kufanya tathmini ya mtu wa mwisho aliyetangamana na mgonjwa aliyekuwa ameambukizwa.
"Kwa kuwa mgonjwa wa mwisho aliyeambukizwa na ugonjwa huo ulioanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliruhusiwa kutoka hospitali Julai 16, kwa hiyo WHO itaanza kufanya tathmini yake kwa siku 42 kuanzia siku hiyo ili kujihakikishia kuwa hakuna msururu wa maambukizi," limeeleza shirika hilo la Afya la Umoja wa Mataifa.
Kumekuwa na maambukizi 3,360 yaliyothibitishwa, vikiwemo vifo 1,487 nchini DRC, mripuko ukiwa mkubwa zaidi katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Ituri.
Uganda, ambayo mpaka wake uko karibu na Ituri, imekuwa na maambukizi 20 yaliyothibitishwa, ikiwemo vifo viwili vilivyothibitishwa, na sasa wagonjwa 18 waliopona…/