-
Africa CDC: Kwa muda wa wiki moja, kesi za Ebola zimeongezeka zaidi ya maradufu mkoani Kasai, DRC
Sep 12, 2025 10:27Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Maradhi, (Africa CDC) kimetangaza kuwa, idadi ya watu wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa hatari wa Ebola katika jimbo la Kasai kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka zaidi ya maradufuu katika muda wa wiki moja tangu ulipothibitishwa mripuko mpya wa ugonjwa huo katika eneo hilo.
-
DRC yatangaza mripuko wa 16 wa Ebola; WHO yatoa indhari
Sep 05, 2025 10:38Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza mripuko mpya wa Ebola katika jimbo la kati la Kasai, ambalo ni la 16 nchini humo tangu 1976, huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likitahadharisha kuwa huenda maambukizi ya maradhi hayo yakaongezeka.
-
Uganda yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola ulioua makumi
Jan 11, 2023 11:15Uganda imetangaza habari ya kudhibitiwa na kutokomezwa mlipuko wa Ebola ambao umeua makumi ya watu nchini humo tangu Septemba mwaka uliomalizika 2022.
-
Afrika CDC: Mlipuko wa Ebola nchini Uganda "unadhibitika"
Oct 27, 2022 13:00Shirika la juu zaidi la afya ya umma barani Afrika (Afrika CDC) limetangaza leo Alhamisi kwamba mlipuko wa Ebola nchini Uganda bado unadhibitiwa, licha ya kuongezeka kwa kesi za maambukizi ya ugonjwa huo hadi katika mji mkuu, Kampala.
-
Afrika CDC: Mripuko wa Ebola Uganda unaweza kudhibitiwa
Oct 21, 2022 04:13Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC) kimesema kuna hatari ya mripuko wa Ebola unaoshuhudiwa nchini Uganda kusambaa katika nchi nyingine, lakini msambao huo unaweza kudhibitiwa hivi sasa.
-
Idadi ya wahanga wa Ebola yazidi kuongezeka Uganda
Oct 19, 2022 08:03Wizara ya Afya ya Uganda imetangaza kuhusu kuongezeka idadi ya watu wanaoga dunia kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo.
-
Uganda yafunga wilaya 2 ili kudhibiti msambao wa Ebola
Oct 16, 2022 11:19Serikali ya Uganda imetangaza habari ya kuziweka wilaya mbili za nchi hiyo katika karantini, kwa lengo la kudhibiti mripuko wa virusi vya Ebola unaoshuhudia katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa.
-
Daktari Mtanzania aaga dunia kwa Ebola nchini Uganda
Oct 01, 2022 12:14Daktari mmoja raia wa Tanzania aliyekuwa akifanya kazi nchini Uganda ameaga dunia kutoka na ugonjwa wa Ebola.
-
DRC yatangaza kumalizika mripuko wa sasa wa Ebola
Sep 28, 2022 08:09Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza habari ya kutokomezwa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa nchi.
-
DRC yafanya kampeni ya chanjo baada ya Ebola kuripotiwa Beni
Aug 25, 2022 12:04Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo Alkhamisi imezindua kampeni ya kutoa chanjo katika mji Beni, mashariki mwa nchi, baada ya kesi ya virusi hivyo kuthibitishwa katika mji huo.