Oct 19, 2022 08:03 UTC
  • Idadi ya wahanga wa Ebola yazidi kuongezeka Uganda

Wizara ya Afya ya Uganda imetangaza kuhusu kuongezeka idadi ya watu wanaoga dunia kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Ebola ni ugonjwa unaoua uliopewa jina la mto mmoja huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao uligunduliwa mwaka 1976. Dalili za ugonjwa huo ni kuwa na homa kali, kutapika, kutoka damu katika matundu mbalimbali ya mwili na kuhara. Wizara ya Afya ya Uganda imetangaza baada ya kuthibitisha vifo vya watu 5 siku nne zilizopita kwamba, hadi sasa watu 254 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo.  

Wizara ya Afya ya Uganda na mikakati ya kuzuia kuenea Ebola 

Imeongeza kuwa, jumla ya watu 60 wameambukizwa Ebola hadi sasa huko Uganda, watu 24 wakiwa wamepata nafuu na 11 wamelazwa kwa ajili ya matibabu. Serikali ya Uganda imezuia kutoka na kuingia katika miji ya Mubende na Kasanda kwa muda wa siku 21 ili kuzuia kuenea maradhi hayo. Mlipuko wa mwisho wa Ebola ulitokea mashariki mwa Kongo mwezi Agosti mwaka 2018 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1,800. 

Tags