Harakati ya M-23: Mazungumzo ya amani na serikali ya Congo yanaendelea
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i133442-harakati_ya_m_23_mazungumzo_ya_amani_na_serikali_ya_congo_yanaendelea
Harakati ya M-23 imethibitisha kwamba mazungumzo na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huko Doha yataendelea katika wiki zijazo.
(last modified 2025-11-21T10:30:19+00:00 )
Nov 21, 2025 10:30 UTC
  • Corneille Nangaa
    Corneille Nangaa

Harakati ya M-23 imethibitisha kwamba mazungumzo na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huko Doha yataendelea katika wiki zijazo.

Mkuu wa ujumbe wa mazungumzo ya amani wa harakati hiyo, Corneille Nangaa, amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari, siku chache baada ya pande hizo mbili kusaini makubaliano ya fremu ya amani, kwamba "mazungumzo hayo yatazingatia masuala muhimu, ikiwa ni pamoja na ufikaji wa misaada ya kibinadamu kwa waathiriwa, dhamana za mahakama na njia za kuachiliwa huru wafungwa."

Alionya kwamba "mapigano yanayoendelea na makundi yenye silaha ya ndani yanaweza kutishia utekelezaji wa makubaliano ya amani."

Mapema wiki hii msemaji wa serikali ya Congo, Patrick Moya alisema kwamba Kinshasa haitakubali kuachia eneo lolote la ardhi ya Congo katika mazungumzo ya Doha, akisisitiza kwamba "umoja wa ardhi ya nchi hauwezi kujadiliwa" na kwamba "serikali imejitolea kurejesha amani mashariki mwa nchi."

Inafaa kukumbusha kwamba wiki iliyopita serikali ya Kongo na harakati ya M-23 walisaini makubaliano ya amani mjini Doha, yaliyosimamiwa na Qatar.