-
Wabunge wa Uganda watilia shaka uamuzi wa serikali kutaka kupeleka wanajeshi Ghaza
Aug 07, 2026 12:27Baadhi ya wabunge wa upinzani nchini Uganda wametilia shaka uamuzi wa serikali wa kutaka kupeleka wanajeshi wa nchi hiyo huko Ukanda wa Ghaza watakaokuwa sehemu ya kikosi cha kimataifa cha kurejesha uthabiti katika eneo hilo la ardhi ya Palestina.
-
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi
Jul 30, 2026 14:53Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, amelazwa hospitalini na hana fahamu baada ya kuziraia akiwa mahakamani jana Jumatano. Hayo ni kwa mujibu wa mkewe na watu wengine wanaozihimiza mamlaka husika nchini Uganda kumwachilia huru baada ya kunyimwa dhamana mara kwa mara.
-
WHO yaonya kuwa Uganda ingali iko katika hatari ya mripuko wa ebola
Jul 30, 2026 10:15Shirika la Afya Duniani, WHO leo limetoa indhari kwa Uganda kwamba ingali iko katika hatari kutokana na mripuko wa ugonjwa wa Ebola ulioenea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Uganda: Kizza Besigye apinga kuwekwa kizuizini katika kesi ya uhaini inayomkabili
Jun 10, 2026 03:46Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, amewasilisha ombi mahakamani akitaka kutolewe uamuzi wa kusimamisha kuendelea kushikiliwa kizuizini na kufunguliwa mashtaka.
-
Ebola imeua watu 139, wengine 600 wameambukizwa DRC na Uganda
May 21, 2026 12:56Takriban wagonjwa 600 sasa wanashukiwa kuwa na Ebola na vifo 139 vikishukiwa kusababishwa na ugonjwa huo hali inayoongeza hofu ya kuenea zaidi kwa mlipuko wa sasa wa Ebola.
-
Uganda yawaweka karantini zaidi ya watu 100 huku WHO ikitoa tahadhari kuhusu kasi ya Ebola
May 20, 2026 03:20Serikali ya Uganda inasema zaidi ya watu 100 wamewekwa karantini huku maafisa wa afya wakijitahidi kudhibiti mlipuko nadra wa Ebola unaohusishwa na aina ya virusi vya Bundibugyo.
-
Uganda yapitisha sheria ya kudhibiti ushawishi wa kigeni
May 18, 2026 12:03Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayolenga kudhibiti ushawishi wa kigeni nchini humo.
-
WHO yaainisha mlipuko wa Ebola Congo DR na Uganda kama dharura ya afya ya umma
May 17, 2026 08:45Shirika la Afya Duniani (WHO) limeainisha mlipuko wa virusi vya Ebola vya Bundibugyo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda kama dharura ya afya ya umma inayotia wasiwasi kimataifa.
-
Mwana wa Rais wa Uganda amuita 'Hitler' kiongozi wa RSF aliyekutana na baba yake hivi karibuni
Feb 24, 2026 07:43Mwana mtatanishi wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye ni mkuu wa majeshi ya nchi hiyo Muhoozi Kainerugaba ametoa matamshi yasiyo ya kawaida katika kumshambulia kiongozi wa wanamgambo wa Sudan wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo ambaye hivi karibuni alikutana na baba yake huko nchini Uganda.
-
Afya ya kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Uganda aliyeko gerezani yadaiwa kuzorota
Jan 20, 2026 23:09Chama cha upinzani nchini Uganda cha People’s Front for Freedom kimesema katika taarifa kwamba afya ya kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo Kizza Besigye “iko katika hali mbaya na inaendelea kudhoofika,” na kutoa mwito wa kutaka aruhusiwe kukaguliwa na madaktari wake binafsi pamoja na familia yake.