-
Kiongozi Mkuu: Ghaza ndiyo mshindi mkuu kwenye medani ya vita na utawala wa Israel mwangamizaji wa kizazi
Mar 29, 2024 00:01Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema vikosi vya Muqawama na watu wa Ghaza ndio washindi kwenye medani ya vita na utawala wa Israel mwangamizaji wa kizazi na akasisitiza kwa kusema: kilele cha kuheshimika na kusimama imara watu wa Ghaza na Palestina na kushindwa utawala wa Kizayuni katika vita hivyo vya miezi sita ni tukio na jambo lenye rehma za Mwenyezi Mungu.
-
Erdogan: Dunia iishinikize Israel itekeleze azimio la Baraza la Usalama la UN
Mar 28, 2024 23:08Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ameitaka jamii ya kimataifa iendelee kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel utekeleze azimio la kutaka kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza, lililopasishwa majuzi na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Wataalamu wa US: Mapigano ya Al-Shifa yanaonyesha wapiganaji Wapalestina wangali wako imara
Mar 28, 2024 06:39Wataalamu wa masuala ya vita wa Marekani wamesema, wapiganaji wa Kipalestina wamefanya mashambulizi yapatayo 70 dhidi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel karibu na hospitali ya al-Shifa katika mji wa Ghaza tangu Machi 18 wakati jeshi la utawala huo ghasibu liliporejea katika eneo hilo.
-
Rais wa Iran: Palestina sasa ni kadhia ya ulimwengu wa ubinadamu
Mar 27, 2024 23:41Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kutokana na muqawama au mapambano ya Kiislamu na misimamo imara ya wananchi wanaodhulumiwa na wenye nguvu wa Gaza, kadhia ya Palestina sasa imevuka mipaka ya ulimwengu wa Kiislamu na kuwa suala la ulimwengu wa ubinadamu.
-
Ulimwengu waunga mkono ripoti ya UN kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel Ukanda wa Gaza
Mar 27, 2024 08:36Tathmini iliyofanywa na Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Palestina ambayo imezitaja jinai za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza kuwa ni mauaji ya kimbari imeungwa mkono pakubwa na nchi mbalimbali katika umoja huo.
-
Soda ya 'Palestine Cola' yazinduliwa, mashirika ya Magharibi yaendelea kususiwa
Mar 26, 2024 22:38Ndugu wawili wa Kipalestina wamezindua soda waliyoipa jina la 'Palestine Cola' na kusema kuwa, faida zote zitakazotokana na mauzo ya kinywaji hicho zitawaendea Wapalestina.
-
Shirikisho la Soka la Iran likaribisha pendekezo la Wapalestina la kuwekewa vikwazo Shirikisho la soka la Israel
Mar 25, 2024 08:14Mkuu wa Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia barua Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), akikaribisha mpango uliopendekezwa wa Shirikisho la Soka la Palestina kuhusu kuwekewa vikwazo Shirikisho la Soka la utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Wairani waandamana kulaani jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza
Mar 24, 2024 23:21Wananchi wa Iran wamefanya maandamano makubwa katika sehemu mbalimbali za nchi ukiwemo mji mkuu Tehran, kutangaza mshikamano na wananchi madhulumu wa Palestina wanaoendelea kuuawa, sambamba na kulaani jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Wapalestina 72 wameuawa shahidi Ukanda wa Gaza katika masaa 24 yaliyopita
Mar 23, 2024 23:22Wizara ya Afya ya Palestina jana ilitangaza kuwa Wapalestina wasiopungua 72 wameuawa shahidi na wengine 114 kujeruhiwa katika masaa 24 yaliyopita kufuatia mauaji ya kimbari yanayondelea kufanywa na Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
-
Israel yapora ekari 2,000 za ardhi ya Wapalestina Ukingo wa Magharibi
Mar 23, 2024 04:10Utawala ghasibu wa Israel umetangaza habari ya kunyakua ekari karibu 2,000 (hektari 800) za ardhi ya Palestina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu.