-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar: Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi halina nguvu yoyote
Jan 13, 2019 03:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (GCC) na Katibu Mkuu wake hawana nguvu yoyote. Mohammed Abdulrahman Aal Thani ameyasema hayo jana katika mazungumzo huko Doha na Abdullatif al Zayan Katibu Mkuu wa baraza hilo na Yusuf bin Alawi Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman.
-
Safari ya saba nje ya nchi ya rais wa Iraq katika siku 100 za mwanzo tangu kuingia madarakani
Jan 11, 2019 04:08Rais Barham Salih wa Iraq siku ya Jumatano ya tarehe 9 Januari aliwasili Doha, mji mkuu wa Qatar kwa safari rasmi ya kuitembelea nchi hiyo.
-
Qatar yautaka Umoja wa Ulaya kuiwekea mashinikizo Saudi Arabia
Dec 21, 2018 05:10Mkuu wa Kamati ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Qatar ameuomba Umoja wa Ulaya kuiwekea mashinikizo zaidi Saudi Arabia ili iondoe vikwazo vyake dhidi ya Qatar.
-
Qatar: Saudi Arabia na Imarati ndio wahatarishaji wakuu wa amani ya Mashariki ya Kati
Dec 17, 2018 23:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ndio wahatarishaji wakuu wa utulivu na usalama wa nchi za Mashariki ya Kati na lengo lao kuu ni kuvunja amani ya nchi zote za eneo hilo.
-
Qatar kuwajengea makazi wakimbizi wa Yemen
Dec 17, 2018 06:03Mfuko wa Maendeleo wa Qatar ambayo ni taasisi ya masuala ya kibinadamu ya nchi hiyo pamoja na Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa zimesaini makubaliano ya kujenga makazi kwa ajili ya raia elfu 26 wa Yemen waliokimbia vita vya miaka minne nchini mwao.
-
Qatar: Baraza la (P)GCC halina uwezo na limebaki limeemewa
Dec 15, 2018 10:56Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar amesema kuwa, Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi limebaki kimuundo tu lakini taratibu zake kiutendaji hazitekelezeki.
-
Qatar yakosoa taarifa ya mwisho ya mkutano wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi
Dec 10, 2018 03:05Qatar imekosoa taarifa ya mwisho ya mkutano wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ikisema kuwa, imeangalia mambo kijuujuu na kuweka kando matatizo ya kweli yanayolikabili baraza hilo.
-
Qatar kujiondoa OPEC Januari 2019
Dec 03, 2018 04:33Qatar imetangaza kuwa itajiondoa katika Shirika la Nchi Zinazouza Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC) mwezi ujao wa Januari 2019.
-
Misri na Saudia zasema mzingiro dhidi ya Qatar utaendelea
Nov 28, 2018 04:11Saudi Arabia na Misri zimesema mzingiro na vikwazo zilivyoiwekea Qatar kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa vitaendelea kwa muda usiojulikana, licha ya Doha kuwasilisha lalama zake mbele ya mahakama za kimataifa na taasisi za Umoja wa Mataifa ili kushinikiza kuhitimishwa mzingiro huo.
-
Baada ya kufeli njama zao sasa viongozi wa Saudia waanza kujipendekeza kwa Qatar
Oct 31, 2018 12:04Mfichuaji mmoja mkubwa wa ufisadia wa utawala wa Aal Saud amefichua kwamba viongozi wa ngazi za juu wa Saudi Arabia wamejipeleka kwa siri nchini Qatar lakini viongozi wa Doha wamewadhalilisha viongozi hao wa Saudia.