-
Baada ya kushindwa njama zao dhidi ya Qatar na Yemen, kundi la Saudia lamalizia hasira zake kwa Uturuki
Dec 20, 2017 12:54Serikali ya Uturuki imekasirishwa sana na hatua ya waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) aliyetuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumtuhumu Rais Recep Tayyip Erdogan kuwa ni kutoka kizazi cha Waturuki waliofanya wizi mjini Madina na kukandamiza Waarabu wakati wa utawala wa Uthmaniyyah (Ottoman Empire).
-
Imarati yakerwa na kuwasilishwa kesi dhidi yake ICC, yailaumu Qatar
Nov 29, 2017 04:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu ameeleza kughadhibishwa kwa Imarati na hatua ya shirika moja la kutetea haki za binadamu kufungua faili la jinai za kivita za nchi hiyo dhidi ya Yemen.
-
Imarati: Muungano wa kijeshi wa Saudia unapaswa kuishambulia kwa bomu al-Jazeera
Nov 26, 2017 09:45Afisa mwandamizi wa usalama wa Umoja wa Falme za Kiarabu ametoa mwito kwa muungano wa kijeshi wa Saudi Arabia kuishambulia kwa bomu kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar.
-
Qatar: Saudia inafanya ukandamizaji ndani ya nchi na uchochezi nje ya nchi
Nov 21, 2017 10:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amekosoa vikali sera ya utawala wa Aal-Saud ya kuwakandamiza wananchi wa Saudi Arabia na wakati huo huo kuzichochea nchi nyingine.
-
Qatar: Uhusiano wetu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni wa "kipekee"
Nov 19, 2017 00:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar ameutaja uhusiano uliopo kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa wa "kipekee".
-
Qatar: Saudia inayakandamiza 'mataifa madogo' kwa lengo la kuyapigisha magoti
Nov 18, 2017 04:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema utawala wa Saudi Arabia unachochea migogoro na mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati sambamba na kuzikandamiza na kuzinyanyasa nchi ndogo katika eneo ili kuzishinikiza zipige magoti mbele yake.
-
Rais Erdoğan aichoma moyo Saudia, asisitiza kuendelea kuiunga mkono Qatar
Nov 16, 2017 04:39Katika kile kinachonekana kuwa ni kuwachoma moyo viongozi wa Saudi Arabia katika mgogogro unaoendelea kati ya nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesisitizia uungaji mkono wake kwa Qatar.
-
Qatar: Tutaimarisha na kulinda uhusiano wetu na Iran
Nov 13, 2017 11:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa, Iran ni nchi jirani na nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na kwamba Doha ina manufaa ya pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivyo haiwezi kukata uhusiano wake na Tehran.
-
Rais wa Uturuki akosoa kauli ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi kuhusu Uislamu
Nov 12, 2017 04:08Katika msururu wa kurushiana maneneo viongozi wa Saudi Arabia na Uturuki, Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki amekosoa vikali matamshi ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia Mohammad Bin Salman kuhusu kile alichodai kuwa ni "Uislamu wa misimamo ya wastani."
-
Amir wa Qatar: Iran ndio njia pekee ya kupitishia chakula na dawa katika kipindi cha mzingiro
Oct 30, 2017 23:16Mfalme wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amesema Iran ndio njia pekee ya kupitishia chakula kwa ajili ya wananchi wa Qatar waliowekewa mzingiro; na akaongeza kwamba Saudi Arabia na nchi nyengine tatu za Kiarabu zinakula njama ya kuubadilisha utawala katika nchi yake.