Pars Today
Hatua ya mtawala wa muda mrefu wa Equatorial Guinea kusema kuwa nchi hiyo itauhamishia ubalozi wake mjini Quds Tukufu unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel kutoka Tel Aviv imekosolewa vikali ndani ya nje ya nchi.
Malawi inatazamiwa kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufuata mkumbo wa Marekani wa kufungua ubalozi katika mji mtukufu wa Quds huko Palestina unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Mahakama moja katika utawala wa Kizayuni wa Israel imetoa amri ya kubomolewa msikiti mmoja ulioko mashariki wa Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa wito wa kuanzishwa kamati ya mirengo yote ya Palestina kwa ajili ya kuutetea mji wa Quds Tukufu (Jerusalem) na kuulinda kutokana na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
"Bila shaka kirusi cha Uzayuni hakitadumu kwa muda mrefu na kwa kutegemea hima, imani, ghera ya vijana, mizizi ya kirusi hicho itang'olewa na kuondolewa katika eneo".
Katibu Mkuu wa chama cha Republican cha Tunisia amesema utawala ghasibu wa Israel hauelewi lugha nyingine isipokuwa ya mapambano na kusisitiza kuwa, "umoja na muqawama ndiyo njia pekee ya kuikomboa Palestina."
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameielezea Siku ya Kimataifa ya Quds inayoadhimishwa hii leo kote duniani kama utamaduni mzuri na nembo ya uvumilivu, umoja na mshikamano wa Waislamu katika kuhami na kutetea thamani za Kiislamu.
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema "Muamala wa Karne" unakusudia kusambaratisha kadhia ya Palestina.
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu yanatazamiwa kufanyika katika ukumbi wa Instagram na mitandao mingine ya kijamii nchini Afrika Kusini, kutokana na janga la corona.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umemkamata Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Wakfu wa Kiislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) huku kukiwa na tetesi kuwa Wazayuni wanalenga kumuambukiza kirusi cha corona.