Sep 15, 2020 07:29 UTC
  • Mahakama ya Israel yatoa agizo la kubomolewa msikiti Quds Mashariki

Mahakama moja katika utawala wa Kizayuni wa Israel imetoa amri ya kubomolewa msikiti mmoja ulioko mashariki wa Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu.

Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini katika Ukanda wa Gaza imelaani vikali uamuzi huo wa mahakama ya Kizayuni, wa kutoa agizo la kubolomewa Nyumba Tukufu ya waumini wa Kiislamu katika mji mtukufu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.

Mahama hiyo ya Kizayuni inadai kuwa, msikiti huo Qaqaa Bin Amr ulioko mjini Silwan umejengwa bila kibali cha ujenzi kutoka kwa utawala huo.

Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini katika Ukanda wa Gaza imeitaka jamii ya kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuyalinda maabadi na maeneo matakatifu ya Kiislamu mjini Quds.

Utawala huo haramu umeshadidisha kampeni ya kubomoa misikiti na nyumba za Wapalestina

Utawala pandikizi wa Israel umewapa wakazi wa mji huo siku 21 kukata rufaa ya kupinga uamuzi huo, vinginevyo agizo hilo la kubomolewa msikiti utekelezwe.

Msikiti huo ambao ulijengwa mwaka 2012, una uwezo wa kubeba mamia ya waumini wa Kiislamu kwa wakati mmoja.

Tags