-
Rais Rouhani aipongeza Tanzania kwa mnasaba wa uhuru wa Tanganyika
Dec 09, 2017 11:51Rais Hassan Rouhani wa Iran amemtumia salamu za pongezi, kheri na fanaka Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika.
-
Rais wa Iran asisitiza juu ya Waislamu kuwa macho na Ubeberu na Uzayuni
Dec 06, 2017 22:13Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa Waiskamu kuwa macho na njama za maadui.
-
Marais wa Iran na Uturuki watoa wito wa kusimama kidete dhidi ya njama mpya huko Palestina
Dec 06, 2017 11:35Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki wametoa wito wa kusimama kidete na kuchukuliwa hatua za maana kwa ajili ya kukabiliana na njama mpya dhidi ya taifa madhulumu la Palestina.
-
Rouhani awapongeza Waislamu kwa Maulidi na siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw)
Dec 06, 2017 01:24Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewapongeza Waislamu kote duniani na kuwapa mkono wa heri na baraka kwa mnasaba wa siku ya leo tarehe 17 Mfunguo Sita Rabiul Awwal, siku aliyozaliwa ndani yake mbora wa viumbe na rehma ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake, Muhammad bin Abdullah (saw).
-
Rais Rouhani: Nguzo kuu za ugaidi katika eneo zimeporomoka
Dec 05, 2017 12:41Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa leo, nguzo kuu za ugaidi katika eneo la Asia Magharibi zimeporomoka na kuongeza kuwa, 'sehemu kubwa ya njama za madola makubwa duniani, uistikabri na Uzayuni dhidi ya mataifa ya eneo zimegonga mwamba.'
-
Rais Rouhani: Bandari ya Chabahar itasafirisha bidhaa kuelekea nchi jirani na Iran kwa gharama nafuu zaidi
Dec 03, 2017 04:52Awamu ya kwanza ya upanuzi wa gati ya bandari ya kimataifa ya Shahidi Beheshti iliyoko Chabahar kusini mashariki mwa Iran imeanza rasmi leo katika hafla iliyohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wawakilishi wa nchi 17 duniani.
-
Rouhani: Uhasama wa Saudia ni mbinu ya kuficha changamoto zinazoikabili
Nov 29, 2017 04:50Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya Saudi Arabia kushadidisha uhasama na uadui wake dhidi ya Tehran ni mbinu ya kujaribu kuficha kufeli kwake katika masuala ya kieneo sawa na changamoto zinazoukabili utawala wa Riyadh ndani ya nchi hiyo.
-
Rais Rouhani: Iran itaendelea kuwa pamoja na Syria katika vita dhidi ya ugaidi
Nov 26, 2017 00:15Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kuendelezwa vita dhidi ya makundi ya kigaidi na kusema kuwa, Iran itaendelea kuwa pamoja na wananchi na serikali ya Syria katika vita dhidi ya ugaidi.
-
Viongozi wa Iran waendelea kulaani shambulizi la kigaidi dhidi ya Waislamu msikitini Misri
Nov 25, 2017 12:50Viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameendelea kulaani vikali shambulizi la kigaidi lililolenga Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala ya Ijumaa msikitini katika eneo la Sinai nchini Misri na kuua mamia ya watu wasio na hatia yoyote.
-
Rais Rouhani: Natija ya kikao cha Sochi ni kuundwa Kongamano la Kitaifa Syria
Nov 23, 2017 00:59Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, natija kuu katika kikao cha Sochi ni kuundwa kongamano la kitaifa la mazungumzo baina ya Wasyria ili kwa njia hiyo, Wasyria kutoka kaumu, dini na madhehebu zote, wakiwemo wapinzani na waungaji mkono wa serikali wakujumuike pamoja kujadili mustakbali wa nchi yao.