Rais Rouhani aipongeza Tanzania kwa mnasaba wa uhuru wa Tanganyika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i37393-rais_rouhani_aipongeza_tanzania_kwa_mnasaba_wa_uhuru_wa_tanganyika
Rais Hassan Rouhani wa Iran amemtumia salamu za pongezi, kheri na fanaka Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 09, 2017 11:51 UTC
  • Rais Rouhani aipongeza Tanzania kwa mnasaba wa uhuru wa Tanganyika

Rais Hassan Rouhani wa Iran amemtumia salamu za pongezi, kheri na fanaka Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika.

Kwa mujibu wa tovuti ya Ofisi ya Rais, Hassan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumamosi amemtumia ujumbe John Magufuli, Rais wa Tanzania kwa mnasaba wa kuwadia siku ya uhuru wa Tanganyika. Katika ujumbe huo, Rais Rouhani amelezea matumaini yake kuwa, kutokana na kuwepo nyanja nyingi za ushirikiano baina ya nchi mbili, pamoja na mitazamo ya pamoja ya nchi mbili katika masuala ya kimataifa, ushirikiano wa Tehran na Dodoma uimarishwe zaidi kwa maslahi ya pande mbili.

Rais Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Rouhani ameitakia serikali na watu wa Tanzania afya, mafanikio na ufanisi. Miaka 56 iliyopita katika siku kama ya leo, yaani tarehe 9 Disemba mwaka 1961 ardhi ya Tanganyika ambayo hii leo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijikomboa na kupata uhuru wake kutoka kwa mkoloni mkongwe wa Ulaya, yaani Uingereza.