Pars Today
Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuhusu faili jipya la mrithi wa ufalme wa Saudia wa kuhusika na jaribio la kumuua afisa wa zamani wa intelijensia wa nchi hiyo aliyekimbilia Canada kuwa, mafaili zaidi ya timu za mauaji za Saudia yako njia na yatafichuliwa karibuni.
Umoja wa Ulaya umeikosoa Saudi Arabia kutokana na kamatakamata na vifungo vya muda mrefu dhidi ya watetezi wa haki za wanawake nchini humo.
Mjumbe wa Kamati ya Uhusiano wa Kigeni ya Bunge la Iraq amesema kuwa bunge hilo na jumuiya za wananchi zinafanya jitihada za kufungua faili la vibaraka wa Saudi Arabia wenye mfungamano na Marekani nchini Iraq.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameukosoa utawala wa Saudi Arabia kwa hatua zake mbaya dhidi ya wanaharakati waliofungwa katika jela za nchi hiyo.
Mfalme wa zamani wa Uhispania, Juan Carlos ameondoka nchini humo na kuelekea kusikojulikana wiki kadhaa baada ya kuhusishwa na ufisadi na kashfa ya kupokea mlungula kutoka kwa mfalme wa zamani wa Saudi Arabia.
Mbunge mmoja nchini Iraq amefichukua kuhusu mpango wa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu wa kutorosha wafungwa katika jela ya al Hoot nchini Iraq
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kuwa na uhusiano mzuri na Saudi Arabia, lakini inasikitisha kuwa, serikali ya Riyadh haitaki kuweko uhusiano ulio sawa baina yake na Iran.
Mapigano kati ya wanamgambo wa Baraza la Mpito linaloungwa mkono na Imarati na wale wanaoungwa mkono na Saudi Arabia katika mkoa wa Abyan kusini mwa Yemen yameshtadi na kupamba moto.
Utawala wa Saudia Arabia, ambao watawala wake kwa muda mrefu wanajinadi kuwa eti ni 'wahudumu wa maeneo mawili matakatifu ya Waislamu ya Makka na Madina' umekosolewa vikali kwa kuruhusu maonyesho ya mavazi ya kifuska katika mji mtukufu wa Madina.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limezitaka nchi nyingine duniani kuiwekea Saudi Arabia mashinikizo ili kuwaachia huru wanaharakati wa kijamii wanawake waliofungwa jela nchini humo.