UN yataka kuachiwa huru wanaharakati wanawake walioko jela Saudi Arabia
(last modified Fri, 10 Jul 2020 03:07:19 GMT )
Jul 10, 2020 03:07 UTC
  • UN yataka kuachiwa huru wanaharakati wanawake walioko jela Saudi Arabia

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limezitaka nchi nyingine duniani kuiwekea Saudi Arabia mashinikizo ili kuwaachia huru wanaharakati wa kijamii wanawake waliofungwa jela nchini humo.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limezitolea wito nchi wanachama wa baraza hilo kabla ya kufanyika kikao cha wakuu wa G-20 huko Riyadh; ziishinikize Saudi Arabia ili iwaachie huru wanaharakati wa kijamii wanawake walioko jela nchini humo. 

Bi Agnes Callamard Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Anayehusika na Mauaji ya Kiholela na Yaliyo Kinyume cha Sheria ameeleza kuwa, Saudi Arabia inapasa kuwaachia huru wafungwa waliohusishwa na masuala ya kimadhehebu na wanaharakati wanawake watetezi wa haki za binadamu ambao wamefungwa jela nchini humo kwa kosa la kudai haki yao ya kuendesha gari. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo,  makumi ya wanaharakati mashuhuri watetezi wa haki za wanawake wa Saudia  walitiwa mbaroni na serikali ya Riyadh mwaka 2018 na kufungwa jela.  Kutiwa mbaroni kwa wanaharakati hao wanawake wa Kisaudia ni sehemu ya siasa za ukandamizaji zinazotekelezwa na Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo; siasa ambazo zimekosolewa pakubwa kwa mara kadhaa na jamii ya kimataifa. Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa, aghalabu ya wanawake walioko jela nchini Saudi Arabia wamekumbwa na mateso na kunajisiwa mara kadhaa.  

Muhammad bin Salman, Mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia 

 

Tags