Pars Today
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia wana nia ya kustawisha na kuimarisha uhusiano wa pande mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian na mwenzake wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Faisal bin Farhan Al Saud, wanatazamiwa kukutana katika mji mkuu wa China, Beijing kesho Alkhamisi.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza na kusifu misimamo ya serikali na wananchi wa Mauritania ya kuunga mkono malengo matukufu ya wananchi wa Palestina.
Baraza la Mawaziri la Saudi Arabia limeidhinisha uamuzi wa serikali ya nchi hiyo kujiunga na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameeleza hofu na wasi wasi alionao juu ya muungano unaoweza kuanzishwa kati ya Iran, Saudi Arabia, China na Russia.
Televisheni ya Saudi Arabia imemnukuu afisa mmoja katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo na kutangaza kuwa Riyadh imeanza mazungumzo na Syria ili kuanza tena kutoa huduma za kibalozi.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria ilitangaza Jumatatu usiku kwamba makubaliano yaliyotiwa saini kati ya Saudi Arabia na Iran yatasaidia kuimarisha usalama katika eneo na pia kutetea kadhia ya Palestina.
Jarida la National Review limeandika kuwa: Makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia ambayo yalifikiwa kwa upatanishi wa China ni kushindwa kukubwa kwa malengo ya sera za nje za Marekani katika eneo la Mashariki mwa Asia.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya imetoa taarifa na kukaribisha mapatano yaliyofikiwa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia na kueleza kuwa, mapatano hayo yana maslahi kwa nchi mbili na eneo zima la Asia Magharibi kwa ujumla.
Ofisi ya ubalozi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imepongeza mapatano ya kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Saudi Arabia na kueleza kuwa, muafaka huo utaharakisha mchakato wa kusitishwa vita na mapigano nchini Yemen.