• Kigali: Mwenyeji wa kikao cha mameya wa miji ya Francophone + Sauti

    Kigali: Mwenyeji wa kikao cha mameya wa miji ya Francophone + Sauti

    Jul 21, 2021 16:00

    Meya wa miji mikuu ya nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa wameyahimiza mataifa wanachama hasa yale yaliyoko kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika kulipa kipaumbele suala la kuwaelimisha wananchi wao kuhusu elimu ya uzazi wa mpango. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.

  • Waandishi Tanzania watakiwa kutumia vizuri kalamu zao kutatua migogoro + Sauti

    Waandishi Tanzania watakiwa kutumia vizuri kalamu zao kutatua migogoro + Sauti

    Jul 15, 2021 13:37

    Waandishi wa habari nchini Tanzania wametakiwa kutumia vizuri kalamu zao kwa ajili ya kuimarisha amani na kutatua migogoro katika jamii ikiwemo ya wakati wa uchaguzi. Harith Subeit na maelezo zaidi kutoka Zanzibar.

  • Rais Mwinyi wa Zanzibar aahidi mazuri zaidi kupitia uchumi buluu + Sauti

    Rais Mwinyi wa Zanzibar aahidi mazuri zaidi kupitia uchumi buluu + Sauti

    Jun 13, 2021 08:02

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa, serikali ya awamu ya nane ya Zanzibar ina dhamira ya dhati ya kupanua wigo wa matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake ili kujenga uchumi wa buluu ulio imara kwa taifa. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit na maelezo zaidi.

  • Hatimaye Jumuiya ya Waislamu Burundi yapata kiongozi mpya + SAUTI

    Hatimaye Jumuiya ya Waislamu Burundi yapata kiongozi mpya + SAUTI

    Feb 08, 2021 16:00

    Jumuia ya Waislamu nchini Burundi (COMIBU) hatimaye imepata kiongozi mpya baada ya kubakia wazi kwa muda wa miezi 5. Kiongozi huyo mpya Sheikh Hassan Nyamweru aliyeshinda uchaguzi kwa asilimia 84 ya kura dhidi ya mpinzani wake Sheikh Salum Nayabagabo aliyepata kura 32. Amida ISSA na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.

  • Mauaji dhidi yao yaongezeka, waandishi wa habari wataka ulinzi zaidi Uganda + SAUTI

    Mauaji dhidi yao yaongezeka, waandishi wa habari wataka ulinzi zaidi Uganda + SAUTI

    Feb 08, 2021 15:53

    Kwa mara nyingine waandishi wa habari nchini Uganda wameiomba Serikali iwape ulinzi wa kutosha ili kuzuia mauaji wanayofanyiwa mara kwa mara na ambayo sasa hivi yamekithiri. Mwandishi wa Kampala Kigozi Ismail na taarifa zaidi:

  • Wanaokaidi karantini ya corona Kigali Rwanda, kukiona + Sauti

    Wanaokaidi karantini ya corona Kigali Rwanda, kukiona + Sauti

    Jan 21, 2021 18:08

    Siku tatu baada ya mji mkuu wa Rwanda Kigali kuwekwa kwenye zuio la wakazi wake kukaa nyumbani, baadhi ya wananchi wameonekana kukaidi miito hiyo na polisi wameonya kuwachukulia hatua kali ikiwa wataendelea kufanya hivyo. Serikali ya Rwanda iliamua kuweka zuio la wiki mbili kwa wakazi wa mji mkuu Kigali kutokana na ongezeko la maambukizi ya kirusi cha corona. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.

  • Vipimo vya COVID-19 kupatikana kwa wingi na rahisi nchini Rwanda + Sauti

    Vipimo vya COVID-19 kupatikana kwa wingi na rahisi nchini Rwanda + Sauti

    Dec 18, 2020 13:25

    Serikali ya Rwanda imeziruhusu zahanati zote binafsi nchini humo kupima maambukizo ya kirusi cha corona tena kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi vinavyotoa majibu chini ya dakika 15. Rwanda inasema inafanya hivyo kukabiliana na kasi ya ongezeko zaidi la wagonjwa wa COVID-19 nchini humo. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.

  • Vita vya kupambana na rushwa vinaendelea nchini Rwanda + Sauti

    Vita vya kupambana na rushwa vinaendelea nchini Rwanda + Sauti

    Dec 10, 2020 16:45

    Serikali ya Rwanda imesema kuwa, utashi wa serikali na mikakati inayoendelea kuwekwa, ndivyo vitakavyokuwa suluhisho la kutokomeza ulaji rushwa nchini humo. Licha ya Rwanda kutajwa na mashirika ya kimataifa kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri kwenye mapambano ya ulaji rushwa lakini bado nchi hiyo inasema juhudi kali za kuikabili rushwa zitaendelea. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi…

  • Mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda aonana na wagombea kutuliza mambo + SAUTI

    Mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda aonana na wagombea kutuliza mambo + SAUTI

    Nov 16, 2020 15:38

    Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Uganda amekutana na wagombea urais wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 Januari 2021 nchini humo, ili kutatua migogoro iliyojitokeza wakati huu wa kampeni za uchaguzi. Maelezo zaidi na mwandishi wetu wa Kampala, Kigozi, Ismail.

  • Matukio ya ulimwengu wa Kiislamu na Harith Subeit + Sauti

    Matukio ya ulimwengu wa Kiislamu na Harith Subeit + Sauti

    Oct 02, 2020 18:41

    Wiki hii pia kama ilivyo kwa wiki zote, ukanda wa Afrika Mashariki na Kati umeendelea kuwa na matukio mengi ya Kiislamu. Mwandishi wetu wa Zanzibar Harith Subeit anatudondolea baadhi yake katika ripoti yake hii...