Hatimaye Jumuiya ya Waislamu Burundi yapata kiongozi mpya + SAUTI
(last modified Mon, 08 Feb 2021 16:00:13 GMT )
Feb 08, 2021 16:00 UTC

Jumuia ya Waislamu nchini Burundi (COMIBU) hatimaye imepata kiongozi mpya baada ya kubakia wazi kwa muda wa miezi 5. Kiongozi huyo mpya Sheikh Hassan Nyamweru aliyeshinda uchaguzi kwa asilimia 84 ya kura dhidi ya mpinzani wake Sheikh Salum Nayabagabo aliyepata kura 32. Amida ISSA na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.