-
Uchambuzi wa Sayyid Hassan Nasrullah juu ya uamuzi wa Ujerumani dhidi ya Hizbullah
May 06, 2020 03:36Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kwamba uamuzi wa Ujerumani wa kuituhumu harakati hiyo kuwa ni ya kigaidi ulitokana na mashinikizo ya Marekani na utawala haramu wa Kizayuni.
-
Nasrullah: Maadui wanataka kuondoa imani ya wananchi kwa kambi ya Muqawama
Mar 21, 2020 03:38Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, maadui wanafanya kila njia ili kuyumbisha imani iliyopo baina ya Muqawama na wananchi, ambao ndio watoaji msukumo halisi kwa mhimili wa muqawama.
-
Sayyid Hassan Nasrullah: Kukabiliana na Marekani ni lazima kuwe kwa pande zote na kuhusishe sekta zote
Feb 16, 2020 12:36Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani ni muhusika wa vita vyote eneo la Asia Magharibi na amesisitiza kuwa, ni lazima kuendesha muqawama katika pande zote kukabiliana na utawala huo wa kibeberu wa Marekani.
-
"Marekani ilivuka mistari yote miekundu kwa kumuua shahidi Jen. Soleimani"
Feb 13, 2020 23:54Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kwa kumuua kigaidi shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ( SEPAH), Marekani ilivuka mistari yote miekundu na kwamba mauaji hayo yamegeuza mahesabu yote katika eneo la Asia Magharibi.
-
Nasrullah: Siku ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani, mwanzo wa historia mpya Mashariki ya Kati + Video
Jan 05, 2020 12:26Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Sayyid Nasrullah: Vikosi vya Muqawama kote duniani kujibu mapigo ya kuuawa shahidi Soleimani
Jan 03, 2020 10:25Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema vikosi vya wanamuqawama kote duniani vina jukumu la kuwaadhibu wale waliohusika na mauaji ya kikatili ya Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Meja Jenerali Qassem Solaimani.
-
Nasrullah: Hizbullah ni tishio kubwa kwa njama za Marekani na Israel
Dec 14, 2019 03:55Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema njama ghalati za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na uwepo na kusimama kidete harakati hiyo ya muqawama.
-
Askofu Mkuu wa Kanisa la Othodoksi la Quds amuunga mkono Sayyid Hassan Nasrullah
Dec 09, 2019 08:53Askofu Mkuu wa Kanisa la Othodoksi katika mji mtukufu wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) Atallah Hanna, ameiunga harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon sambamba na kulaani matamshi yaliyotolewa na Askofu wa Kanisa la Othodoksi katika mji mkuu wa nchi hiyo Beirut, ya kuitusi harakati hiyo na Katibu Mkuu wake Sayyid Hassan Nasrullah.
-
Nasrullah: Hizbullah inatekeleza jukumu lake, Marekani inazuia utatuzi Lebanon
Nov 02, 2019 00:49Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon jana Ijumaa alitoa hotuba muhimu katika kumbukumbu za kumuenzi Allama Sayyid Murdha al Amili, mmoja wa maulamaa na wanavyuoni wakubwa wa nchini Lebanon, na mbali na kugusia shakhsia ya mwanachuoni huyo, amezungumzia pia matukio ya ndani ya Lebanon na kujiuzulu waziri mkuu wa nchi hiyo.
-
Sayyid Hassan Nasrullah: Maadui wamejawa hofu kwa kushuhudia matembezi ya Arubaini
Oct 19, 2019 10:06Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, uwepo wa mamilioni ya watu mjini Karbala ni jambo lisilo na mfano katika historia na kwamba Marekani, utawala haramu wa Kizayuni, mabeberu na madhalimu wa dunia wanahisi hofu kubwa kwa kushuhudia matembezi ya mamilioni ya watu katika Arubaini ya Imam Hussein (as).