-
UNHCR: Watu elfu nne wameuliwa Darfur, Sudan, mali za raia zimeharibiwa
Oct 18, 2023 00:20Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema, watu wapatao 4,000 wameuawa huku mali za raia zikiharibiwa katika mapigano yanayoendelea huko jimboni Darfur nchini Sudan, mapigano ambayo yalianzia kwenye mji mkuu Khartoum miezi sita iliyopita na kusambaa hadi nje ya mji huo, kati ya Jeshi la Serikali (SAF) na wanamgambo wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF).
-
Salva Kiir kuwa mwenyeji wa viongozi wa Sudan kujadili amani
Oct 17, 2023 10:42Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema karibuni hivi atakuwa mwenyeji wa mkutano utakaowaleta pamoja viongozi wa pande mbili zinazopigana nchini Sudan, yaani Jeshi la Taifa la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)
-
Iran na Sudan kufungua tena balozi zao baada ya kukamilisha mchakato wa kuhuisha uhusiano
Oct 10, 2023 03:34Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, karibuni hivi Iran na Sudan zitafungua tena balozi zao baada ya nchi hizo mbili kukamilisha mchakato wa kurejesha uhusiano wa kidipolmasia.
-
UN: Mapigano Sudan yanasababisha kuongezeka kwa kasi mgogoro wa wakimbizi duniani
Oct 05, 2023 23:57Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu huko Sudan amesema kuwa mapigano yanayoendelea nchini humo yanapelekea kuongezeka haraka mgogoro unapanuka wa wakimbizi duniani.
-
Sudan Kusini: Benki ya BRICS ni mwanzo wa mwisho wa udhibiti wa sarafu ya dola
Sep 30, 2023 12:14Waziri wa Mambo ya Rais wa Sudan Kusini amesema kuwa, kudhihiri kwa Benki mpya ya NDB ya kundi la madola yanayoinukia kiuchumu la BRICS utakuwa mwanzo wa kusambaratika udhibiti wa sarafu ya dola ya Marekani katika miamala ya kifedha duniani kote.
-
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC: Najisikia aibu hatujafanya kazi nzuri huko Sudan
Sep 27, 2023 23:29Karim Khan, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amezungumza na televisheni ya France 24 pambizoni mwa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York akikiri kwamba taasisi hiyo haijafanya kazi nzuri kuhusiana na yanayojiri nchini Sudan.
-
OCHA: Mamilioni ya Wasudan wamekuwa wakimbizi kutokana na kuendelea vita na mapigano
Sep 23, 2023 23:45Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa mamilioni ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao na kuwa wakimbizi kutokana na kuendelea vita na mapigano kati ya Jeshi na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, RSF nchini Sudan.
-
Ethiopia: Tumeanza duru mpya ya mazungumzo na Misri na Sudan kuhusu Bwawa Kuu la Renaissance
Sep 23, 2023 10:38Ethiopia imesema imeanza duru ya pili ya mazungumzo na Misri na Sudan kuhusu bwawa lenye utata lililojengwa na nchi hiyo kwenye mto Nile na kuwa chanzo cha mvutano wa muda mrefu kati ya mataifa hayo matatu.
-
Madhara ya kuendelea vita baina ya majenerali wa kijeshi nchini Sudan
Sep 23, 2023 02:54Licha ya kupita miezi mingi, lakini ndio kwanza vita baina ya majenerali wa kijeshi vinaendelea nchini Sudan na hali ya kisiasa na kiuchumi ya nchi hiyo inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku. Cha kusikitisha ni kuwa pamoja na hali kuwa mbaya kiasi hicho, lakini bado pande hasimu zinaendelea kufanya ukaidi wa kutokubali kusimamisha mapigano.
-
Al-Burhan: Vita vya Sudan huenda vikaenea Afrika Mashariki
Sep 23, 2023 00:34Jenerali Abdul Fattah al-Burhan, mkuu wa baraza la uongozi la Sudan ameuonya Umoja wa Mataifa kuwa, vita vinavyoendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika yumkini vitatanuka zaidi na kuenea katika nchi za Afrika Mashariki.