Pars Today
Shirika rasmi la Habari la Sudan (SUNA) limeripoti kuwa watu 11 wamefariki dunia na wengine 60 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko katika mji wa Abu Hamad kaskazini mwa Sudan. Mvua hiyo imebomoa makumi ya nyumba huku timu za uokoaji zikiendelea kusaka watu waliotoweka na wengine walionasa chini ya vifusi.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka baada ya tatizo la njaa kuyaathiri baadhi ya maeneo ya Darfur. Shirika la FAO limeeleza haya katika ripoti yake ya karibuni kuhusu tathmini ya usalama wa chakula.
Jeshi la Sudan limetangaza kuwa kamanda wake mkuu, Jenerali Abdel-Fattah al Burhan amenusurika katika shambulio la ndege mbili sisizo na rubani (droni) katika hafla ya wahitimu wa jeshi. Watu watano wameuawa katika hujuma hiyo ya droni mashariki mwa Sudan.
Pande zinazozozana huko Sudan zimeshiriki katika ukatili mkubwa wa kingono na kijinsia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
Kwa akali watu 22 wameuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa el-Fasher, jimboni Darfur, magharibi mwa Sudan.
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha huko mashariki mwa Sudan imezidisha mateso ya watu waliokimbia makazi yao haswa katika miji ya Gedaref, Kassala na Halfa Aj Jadeedah.
Baada ya kupita zaidi ya mwaka mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan, karibu theluthi moja ya waliojeruhiwa ni wanawake au watoto walio na umri wa chini ya miaka 10. Ripoti hii imeelezwa na Shirika la Misaada ya Kimatibabu la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF).
Mkutano wa makundi ya kisiasa na kiraia ya Sudan ulimalizika jana mjini Cairo, Misri ambapo vyama vya Sudan vilijadili njia za kutatua mgogoro wa ndani wa nchi hiyo, huku baadhi ya makundi yakikataa kutia saini taarifa ya mwisho ya mkutano wa Cairo.
Watu wanane wa familia moja wameripotiwa kuuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na wapiganaji wa kundi la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) magharibi mwa Sudan.
Malik Agar, Makamu wa Rais wa Baraza la Utawala wa Sudan, ameonya juu ya hatari ya kuporomoka kwa Sudan, ambayo haitakuwa kwa nchi hiyo pekee, bali athari zake mbaya zitaenea katika nchi jirani na kwingineko.