-
Sudan: RSF imeua raia wengine 32 El-Fasher, Darfur Kaskazini
Apr 12, 2025 11:39Jeshi la Sudan limesema kwa uchache raia 32 wameuawa katika shambulio jipya la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El-Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini.
-
Sudan yaiambia ICJ kuwa UAE inachochea mauaji ya halaiki Darfur
Apr 11, 2025 02:06Sudan iliiambia Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) jana Alhamisi kwamba, Umoja wa Falme za Kiarabu umekiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari kwa kuunga mkono vikosi vya wanamgambo huko Darfur, na kuwataka majaji wa mahakama hiyo kutoa amri ya dharura ya kuzuia mauaji ya kimbari katika eneo hilo.
-
Mapigano makali yaripotiwa jeshi la Sudan likizilenga ngome za mwisho za RFS huko Khartoum
Apr 05, 2025 07:03Jeshi la Sudan jana Ijumaa lilikabiliana vikali na hasimu wake yaani Kikosi cha Wanamgambo wa Msaada wa Haraka (RSF) katika ngome za mwisho za kikosi hicho katika mji wa Omdurman huko Khartoum.
-
Watu 89 wauawa katika mashambulizi ya RSF Omdurman, Sudan
Apr 03, 2025 07:06Raia wasiopungua 89 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwenye vijiji vya Omdurman, karibu na ufukwe wa Mto Nile, kaskazini magharibi mwa Khartoum, mji mkuu wa Sudan.
-
RSF yaua na kujeruhi makumi ya raia wa Sudan Kordofan Kusini
Apr 03, 2025 02:32Kwa akali raia 12 wa Sudan wameuawa katika mashambulizi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika Jimbo la Kordofan Kusini.
-
Watu 54 wameuawa katika shambulio la anga linalodaiwa kufanywa na jeshi la Sudan
Mar 26, 2025 07:45Makundi ya misaada ya kibinadamu yameripoti kuwa watu wasiopungua 54 wameuawa katika shambulio la anga la jeshi katika soko moja mashariki mwa nchi hiyo.
-
RSF yaua raia 45 Al-Malha; jeshi la Sudan lasonga mbele
Mar 23, 2025 10:55Zaidi ya raia 45 wameuawa katika shambulio la Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika eneo la Al-Malha, yapata kilomita 210 kaskazini mwa El Fasher, magharibi mwa Sudan.
-
Mashambulizi ya RSF magharibi mwa Khartoum yauwa raia 4 na kujeruhi wengine 30
Mar 17, 2025 11:53Mamlaka ya serikali za mitaa huko Sudan imetangaza leo Jumatatu kuwa mashambulizi ya mizinga ya wanamgambo wa kikosi cha RSF yameua raia wanne na kujeruhiwa wengine 30 katika mji wa Omdurman unaopatikana katika jimbo la Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo.
-
Wawakilishi wa Sudan na UAE walumbana katika mkutano wa Baraza la Usalama
Mar 14, 2025 13:02Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York uliokuwa ukichunguza hali ya kibinadamu nchini Sudan umeambatana na malumbano na shutuma za pande mbili kati ya wawakilishi wa Sudan na UAE katika Umoja wa Mataifa.
-
UN: Zaidi ya watu milioni 30 nchini Sudan wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu
Mar 13, 2025 07:43Zaidi ya watu milioni 30 katika nchi iliyoathiriwa na vita ya Sudan wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu huku hali ya maisha ikizidi kuwa mbaya. Haya yalielezwa jana Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).