-
Waislamu Uingereza walalamikia chuki dhidi ya Uislamu katika chama tawala cha Conservative
Jun 06, 2018 23:09Zaidi ya misikiti 350 na jumuiya za Kiislamu nchini Uingereza zimetaka uchunguzi ufanyike kuhusu chuki dhidi ya Uislamu miongoni mwa wanachama wa ngazi za juu wa chama tawala cha Conservative.
-
Waingereza wahamakishwa na gharama kubwa katika harusi ya Mwanamfalme
May 20, 2018 03:45Wananchi wa Uingereza wameghadhabishwa mno na gharama kubwa za harusi ya Mwanafalme wa nchi hiyo, Harry na muigizaji wa Marekani, Meghan Markle iliyofanyika jana Jumamosi.
-
Wananchi wa Uingereza: Tutaandamana dhidi ya Trump
Apr 27, 2018 03:34Makumi ya maelfu ya wananchi wa Uingereza wametangaza kuwa wapo tayari kushiriki katika maandamano dhidi ya ziara ya Rais Donald Trump wa Mareani mjini London.
-
Nyaraka za maktaba ya taifa Qatar zafichua utegemezi aliokuwa nao mwasisi wa Saudia kwa UK
Apr 19, 2018 03:13Tovuti ya maktaba ya taifa ya Qatar imeonyesha nyaraka ilizopokea kutoka maktaba ya Uingereza zinazofichua kuhusu utegemezi aliokuwa nao Abdulaziz Aal Saud, mwasisi wa utawala wa Saudi Arabia kwa dola la kikoloni la Uingereza.
-
Russia: Madai ya shambulizi la silaha za kemikali Syria yaliratibiwa na majasusi wa Uingereza
Apr 17, 2018 09:54Mwakilishi wa Russia katika Shirika Linalopiga Marufuku Matumizi ya Silaha za Kemikali (OPCW) amesema madai ya kutumiwa silaha za kemikali katika eneo la Douma nchini Syria na yaliyotumika kama kisingizio cha kuishambulia nchi hiyo ya Kiarabu, ni operesheni ya mchezo mchafu iliyopangwa na kutekelezwa na asasi za kijasusi za Uingereza.
-
Korea Kaskazini: Hatua ya Uingereza kutuma meli za kijeshi eneo la Korea ni sawa na kututangazia vita
Apr 16, 2018 12:51Serikali ya Korea Kaskazini imeonyesha kukasirishwa na hatua ya Uingereza ya kutuma meli zake za kivita katika Rasi ya Korea na kuitaja hatua hiyo kuwa ni sawa na kutangaza vita.
-
Iran, Russia zatoa onyo kali baada ya US, UK na Ufaransa kuvurumisha makombora Syria
Apr 14, 2018 02:45Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia zimelaani vikali mashambulizi ya makombora ya Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Syria huku zikitoa onyo kali juu ya matokeo mabaya ya hujuma hiyo ya kijeshi dhidi ya nchi huru.
-
Jeshi la Syria lateka na kuwashikilia wanajeshi vamizi wa Uingereza Ghouta Mashariki
Apr 11, 2018 22:02Shirika rasmi la habari la Syria limetangaza kuwa wanajeshi kadhaa wa Uingereza wanashikiliwa mateka kufuatia operesheni iliyofanywa na jeshi la Syria huko Ghouta Mashariki katika viunga vya Damascus.
-
Chama cha Leba cha UK chalaani ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina
Apr 08, 2018 03:10Jeremy Corbyn, Kiongozi wa Chama cha Leba cha nchini Uingereza amelaani vikali kimya cha nchi za Magharibi mbele ya mauaji ya makumi ya Wapalestina yaliyofanywa na vikosi katili vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika mpaka wa Ghaza.
-
White House yahamakishwa na hatua ya Russia kutimua wanadiplomasia 60 wa US
Mar 30, 2018 10:34Ikulu ya Marekani ya White House imeeleza kughadhibishwa kwake na hatua ya Russia kuwafukuza nchini humo makumi ya wanadiplomasia wa Marekani sambamba na kuagiza kufungwa ofisi ya ubalozi mdogo wa nchi hiyo.