-
UN: Kombora la balestiki la Korea Kaskazini limetumika kushambulia mji wa Kharkiv, Ukraine
Apr 30, 2024 03:51Wachunguzi wa vikwazo wa Umoja wa Mataifa wameiambia kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la umoja huo kuwa, mabaki ya kombora yaliyopatikana katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine mnamo Januari 2 yanatokana na kombora la balestiki la Korea Kaskazini aina ya Hwasong-11.
-
UN yaunga mkono maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani ya kuwatetea watu wa Gaza
Apr 28, 2024 00:56Stephen Dujaric Msemaji wa Umoja wa Mataifa jana Ijumaa alisema katika radiamali yake kwa maandamano yanayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu huko Marekani katika kuwaunga mkono watu wa Gaza na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo hilo kwamba: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mfuasi na mungaji mkono mkubwa wa uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na huko Marekani; na anaunga mkono haki ya wananchi ya kufanya maandamano kwa amani.
-
UN: Hali mashariki mwa DRC inatisha na kuna hatari ya mzozo kusambaa kikanda
Apr 25, 2024 06:47Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Maziwa Makuu amewasilisha kwa Baraza la Usalama taswira ya kutisha ya hali ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, inayoambatana na mvutano unaoendelea kati ya nchi hiyo na Rwanda, na hatari ya mzozo huo kusambaa kikanda.
-
Kamishna wa UN: Picha ya mtoto anayetolewa kwenye fuko la mama yake anayekata roho Ghaza ni zaidi ya tukio la vita
Apr 23, 2024 23:14Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amekemea vikali mashambulio ya kinyama na ya mfululizo yaliyofanywa hivi karibuni na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda Gaza na kuua zaidi wanawake na watoto.
-
UN: Moto wa vita vya Sudan unachochewa na silaha zitokazo nje za wakiukaji wa vikwazo
Apr 20, 2024 07:11Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kisiasa na Ujenzi wa Amani, Rosemary Anne DiCarlo ameliambia Baraza la Usalama kwamba vita nchini Sudan vimesababisha "hali mbaya ya kiwango cha kipekee" inayochochewa na silaha kutoka kwa waungaji mkono wa kigeni ambao wanaendelea kukiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa
-
Katibu Mkuu wa UN: Mahesabu mabaya Asia Magharibi yatasababisha janga kwa dunia
Apr 19, 2024 23:29Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu hali ya sasa katika eneo la Asia Magharibi na kusisitiza kuwa, kosa moja la kimahesabu yumkini likasababisha maafa kwa eneo hilo na dunia nzima kwa ujumla.
-
UN yatahadharisha kuhusu ongezeko la magonjwa ya kuambukiza katika Ukanda wa Gaza
Apr 13, 2024 08:21Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema: magonjwa ya kuambukiza yanaenea katika Ukanda wa Gaza kutokana na ukosefu wa maji salama na kuongezeka kwa joto.
-
Mwakilishi wa Iran UN: Marekani imetumia unafasi yake kuunga mkono mauaji ya kimbari huko Gaza
Apr 09, 2024 08:41Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Marekani imetumia sifa na nafasi yake kuunga mkono mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.
-
Watoto ndio wahanga wakuu wa vita vya Gaza
Apr 08, 2024 22:48Katika siku za hivi karibuni vyombo tofauti vya Umoja wa Mataifa vimechapisha ripoti mpya kuhusu kuharibika zaidi hali ya kibinadamu huko Gaza hususan ya watoto, jambo ambalo linaifanya kadhia ya jinai za kivita za jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kupata uzito zaidi.
-
CAIR: UN ichunguze jeshi la Israel lilivyowaua Wapalestina bila sababu na kuzifukia maiti zao
Mar 28, 2024 06:39Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani [CAIR] limetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchunguza video inayoonyesha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakiwapiga risasi bila sababuu Wapalestina wawili wanaoonekana kuwa hawana silaha kisha kuzifukia maiti zao kwa buldoza.