-
Mauaji ya familia ya Kiislamu nchini Canada, nembo ya Islamophobia katika nchi za Magharibi
Jun 09, 2021 11:30Kufuatia mauaji ya kikatili ya familia moja ya Kiislamu kwenye mji wa London katika jimbo la Ontario nchini Canada, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau amesema anahidi kuwa, atachukua hatua zaidi za kukabiliana na makundi yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia.
-
Wanaharakati: UN itambue mauaji ya Mashia Afghanistan kuwa ni mauaji ya kimbari
May 20, 2021 02:35Wanaharakati wa haki za binadamu na utamaduni nchini Afghanistan wameutaka Umoja wa Mataifa utambue rasmi mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Afghanistan katika miaka ya hivi karibuni kuwa ni mauaji ya kimbari.
-
30 wahukumiwa kifo Congo DR kwa kuhusika na ghasia za siku ya Idul Fitri
May 15, 2021 14:25Watu thelathini wamehukumiwa kifo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kesi isiyosikilizwa katika siku moja tu, kwa kupatikana na hatia ya kuhusika na ghasia dhidi ya polisi wakati wa ibada ya Swala ya Idul Fitri ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani katika mji mkuu wa nchi hiyo.
-
Kupasishwa marufuku ya hijabu kwa wafanyakazi wa serikali katika Bunge la Ujerumani
May 12, 2021 00:44Baraza la Juu la Bunge la Ujerumani (Bundesrat) limepasisha sheria inayowapiga marufuku wafanyakazi wa serikali na polisi kuvaa vazi la hijabu.
-
China yapinga unafiki wa Marekani, yasema Washington imeua Waislamu wengi dunia
May 11, 2021 17:12China imepinga unafiki wa Merekani katika madai yake ya kutetea haki za Waislamu waliowachache katika eneo la Magharibi mwa China la Xinjiang, na kusisitiza kuwa, Marekani imeua Waislamu wengi katika vita na operesheni zake za kijeshi kuliko nchi nyingine yoyote duniani.
-
Utafiti: Idadi ya Waislamu imeongezeka nchini Ujerumani
Apr 29, 2021 12:10Uchunguzi uliofanywa na Idara ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Ujerumani umebaini kuwepo ongeseko kubwa la idadi ya Waislamu nchini humo katika miaka ya karibuni.
-
CAIR: Manyanyaso dhidi ya Waislamu yaliongezeka kwa asilimia 9 nchini Marekani mwaka uliopita
Apr 27, 2021 07:44Kundi linaloongoza kwa kutetezi haki za Waislamu nchini Marekani lilitangaza Jumatatu ya jana kwamba kumekuwepo ongezeko la asilimia 9 ya idadi ya malalamiko ya unyanyasaji dhidi ya Waislamu ambayo yalipokewa mwaka uliopita wa 2020 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.
-
Kukiri Biden juu ya kuudhiwa na kubughudhiwa Waislamu nchini Marekani
Apr 14, 2021 02:22Rais Joe Biden wa Marekani amekiri katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuwadia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani juu ya kuudhiwa na kubughudhiwa Waislamu katika jamii ya Marekani.
-
Naim Qassim: Kushikamana Waislamu kumesambaratisha njama za US-Israel
Apr 01, 2021 10:35Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuungana na kushikamana Waislamu pasina kujali tofauti zao za kimitazamo na kiitikadi kumesambaratisha njama za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel za kuyagawanya vipande vipande mataifa ya Kiislamu.
-
Sri Lanka kupiga marufuku niqab, kufunga shule zaidi ya 1,000 za Kiislamu
Mar 14, 2021 08:07Katika kile kinachoonekana ni mwendelezo wa kushtadi chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini Sri Lanka, serikali ya nchi hiyo imetangaza kuwa karibuni hivi itapiga marufuku uvaaji wa vazi la staha la burqa (niqabu) ambalo huvaliwa na baadhi ya wanawake wa Kiislamu.