Utafiti: Idadi ya Waislamu imeongezeka nchini Ujerumani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i69582-utafiti_idadi_ya_waislamu_imeongezeka_nchini_ujerumani
Uchunguzi uliofanywa na Idara ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Ujerumani umebaini kuwepo ongeseko kubwa la idadi ya Waislamu nchini humo katika miaka ya karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 29, 2021 07:40 UTC
  • Utafiti: Idadi ya Waislamu imeongezeka nchini Ujerumani

Uchunguzi uliofanywa na Idara ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Ujerumani umebaini kuwepo ongeseko kubwa la idadi ya Waislamu nchini humo katika miaka ya karibuni.

Utafitii huo ulifanyika kwa kushirikiana an Wizara ya Mambo ya ndani ya Ujerumani chini ya nwani: "Maisha ya Waislamu nchini Ujerumani mwaka 2020" unaonyesha kuwa, kuna Waislamu milioni 5.3 hadi milioni 5.6 nchini humo na kwamba kiasi hicho ni sawa na asilimia 6.4 hadi 6.7 ya jamii yote ya Wajerumani. Utafiti huo unasema idadi ya Waislamu nchini Ujerumani imeongezeka kwa watu laki tisa ikilinganishwa na matokeo ya uchunguzi uliofanyika mwaka 2015.

Idadi ya Waislamu wenye asili ya Uturuki nchini Ujerumani inafikia milioni 2.5 sawa na asilimia 45 ya Waislamu wote wa nchi hiyo.

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa Waislamu milioni 1.5 wa Ujerumani waliwasili nchini humo kutokea katika nchi zinazozungumza lugha ya Kiarabu wakiwemo asilimia 19 kutoka Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.

Pew: Uislamu, dini inayostawi kwa kasi zaidi duniani

Uchunguzi uliofanywa na kituo cha utafiti cha Pew Research Center cha Marekani unaonyesha kuwa, Uislamu ndiyo dini kubwa inayokuwa na kuongezeka kwa kasi duniani ikilinganishwa na dini nyingine.

Kituo hicho cha utafiti cha Marekani kimesema katika ripoti yake kwamba, hadi kufikia mwaka 2070, Uislamu utakuwa ndiyo dini kubwa zaidi ulimwenguni.