-
Ripoti: Israel inashikilia miili 766 ya Wapalestina tangu Oktoba 2023
Feb 03, 2026 07:56Mamlaka za Israel zinashikilia miili ya Wapalestina 766 waliokwishatambuliwa, huku karibu nusu ya miili hiyo ikishikiliwa tangu Oktoba 2023, wakati Israel ilipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro.
-
Waandamanaji Stockholm walaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza licha ya usitishaji vita
Jan 25, 2026 11:12Wananchi wa Sweden wamefanya maandamano mengine katika mji mkuu wa nchi hiyo, Stockholm, kulaani mashambulizi ya Israel yanayowalenga Wapalestina katika Ukanda wa Gaza licha ya kufikiwa mapatano ya usitishaji vita.
-
Itifaki ya kimataifa kuhusu haki ya Wapalestina ya kujiainishia hatima yao
Dec 19, 2025 02:18Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) limeunga mkono haki ya Wapalestina ya kujiainishia hatima na mustakabali wao.
-
Azimio jipya la Baraza Kuu la UN; Msimamo wa kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni
Dec 14, 2025 02:06Sambamba na Israel kukiuka usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio jipya linaloitaka Tel Aviv kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu eneo hilo la Palestina.
-
UN yalaani sera ya Israel ya mateso ya kupangwa dhidi ya Wapalestina
Nov 30, 2025 12:42Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mateso (CAT) imeulaani utawala wa Israel kwa kutekeleza sera ya "mateso ya kupangwa" dhidi ya Wapalestina.
-
Wanajeshi wa Israel waendeleza mashambulizi Ukingo wa Magharibi; Wapalestina 2 wajeruhiwa
Oct 14, 2025 12:50Takriban Wapalestina wawili wamejeruhiwa wakati wanajeshi wa Israel walipovamia na kuwafyatulia risasi wakazi wa eneo la Ukingo wa Magharibi. Wanajeshi wa Israel usiku wa kuamkia leo walivamia pakubwa vijii na miji kadhaa ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
-
Wimbi jipya barani Afrika la kuunga mkono Palestina na kulaani Israel
Sep 30, 2025 12:34Wananchi na viongozi wa nchi za Kiafrika wamelaani jinai za Israel katika wimbi jipya la kuwaunga mkono Wapalestina.
-
Sababu zilizoifanya Colombia itoe wito wa aina yake wa kuundwa jeshi la kimataifa la kuikomboa Palestina
Sep 26, 2025 02:26Colombia imetoa wito wa kuundwa jeshi la kimataifa la kukabiliana na utawala wa kizayuni wa Israel.
-
UNRWA: Zaidi ya wakimbizi laki moja wa Gaza hawajapokea msaada wowote tangu miezi 6 iliyopita
Sep 11, 2025 11:04Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza kuwa, zaidi ya watu laki moja wanaendelea kutaabika na njaa katika maeneo ya kuwahifadhi wakimbizi ya shirika hilo huko Gaza, na hakuna msaada wa kibinadamu ambao umeruhusiwa kuingia katika eneo hilo kwa zaidi ya miezi 6 sasa.
-
Rekodi za Israel: Asilimia 75 ya Wapalestina waliokamatwa Ukanda wa Gaza ni raia
Sep 05, 2025 02:20Takriban asilimia 75 ya Wapalestina waliokamatwa na majeshi ya Israel Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro ni raia. Hii ni kwa mujibu wa data za jeshi la Israel.