Mar 17, 2022 06:38
Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliwasili mjini Moscow siku ya Jumanne akiongoza ujumbe wa ngazi za juu kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Sergey Lavrov, Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Russia kuhusu masuala ya pande mbili, mazungumzo ya Vienna, Ukraine, Syria, Yemen na Afghanistan.