Jun 14, 2020 03:22
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, madai kwamba makombora yaliyotumika kushambulia taasisi za mafuta za Saudi Arabia ARAMCO yana asili ya Iran, hayana msingi wowote na kuongeza kuwa, inasikitisha kuona kwamba sekretarieti ya Umoja wa Mataifa imeonesha kivitendo kuwa inaathiriwa na vitisho vya Marekani.