Oct 09, 2023 15:03 UTC
  • Mapambano yanaendelea kwa siku ya tatu, Hamas yapiga Ashkelon na Ashdod

Mapigano kati ya wapigania ukombozi wa Palestina na jeshi la utawala vamizi wa Israel yameendelea leo kwa siku ya tatu katika maeneo ya ndani ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ukanda wa Gaza, ukiwa mwendelezo wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas) dhidi ya uvamizi wa Israeli, huku kukiwa na makadirio kwamba Wazayuni wasiopunguau 1,000 wa Israeli wameangamizwa hadi sasa.

Jeshi la Israel limekiri kuwa vikosi vyake bado vinapigana na wanaharakati wa Kipalestina katika nukta 7 au 8 karibu na Ukanda wa Gaza.

Mapigano makali yameripotiwa baina ya Wapalestina na wanajeshi wa Israel katika mji wa Sderot, na Idhaa ya 12 ya Israel imeripoti kuwa makabiliano yanaendelea karibu na makutano ya Gevim katikati mwa mji huo.

Jeshi la Israel limekiri kwamba makumi ya askari wake wanashikiliwa mateka na wapiganaji wa Kipalestina na kwamba mamia ya wengine wameuawa katika Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa.

Askari wa Israel wakiwa katika hali mbaya

Wakati huo huo ndege za kivita za Israel zimeendelea kushambulia makazi ya raia katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.

Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, mashambulizi hayo ya ndege za kivita za Israel yanalenga majengo ya raia huko Beit Hanoun, ambapo idadi ya mashahidi imefikia 19, na kwamba nyumba moja ya Wapalestina imelipuliwa huko Khan Yunis, katika shambulizi lililoua watu 5.

Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, idadi ya wahanga wa mashambulizi ya jeshi la Israel imeongezeka na kufikia mashahidi 560 na wengine zaidi ya 2,900 wamejeruhiwa.

Mkurugenzi wa kitengo cha magari ya wagonjwa katika Ukanda wa Gaza ameiambia Al Jazeera kwamba wafanyakazi 5 wa ambulensi wameuawa shahidi, na kuongeza kuwa idadi kubwa ya Wapalestina wameuawa kutokana na mashambulizi ya Israel.

Amesema: "Tunakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu ambayo Gaza haijashuhudia kwa miaka 20."

Kwa upande mwingine wapiganaji wa harakati ya Hamas wameshambulia vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vya Sderot, Ashkelon na Ashdod kwa zaidi ya roketi 90.

Tags