HAMAS yaipongeza Yemen; San'a yasema: Hatutosita kukamata meli yoyote ya Wazayuni
(last modified Mon, 20 Nov 2023 14:53:20 GMT )
Nov 20, 2023 14:53 UTC
  • HAMAS yaipongeza Yemen; San'a yasema: Hatutosita kukamata meli yoyote ya Wazayuni

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeipongeza Yemen na jeshi lake kwa hatua yao ya kishujaa ya kukamata meli ya utawala wa Kizayuni na kusema kuwa hatua hiyo ni mafanikio ya aina yake yaliyopatikana kutokana na damu za watu wasio na hatia zinazomwagwa na Israel huko Ghaza.

Jana Jumapili, jeshi la majini la Yemen lilikamata meli ya utawala wa Kizayuni kwenye Bahari Nyekundu ikiwa na watu 52 ndani yake.

Shirika la habari la Shahab limemnukuu Sami Abu Zuhri, mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS akisema kuwa, Marekani na utawala wa Kizayuni lazima walipe hasara za damu wanazomwaga huko Ghaza.

Amesema: Hatua ya kishujaa ya jeshi la Yemen ya kukamata meli ya utawala wa Kizayuni inapaswa kuwa kigezo kwa umma mzima wa Kiislamu ili popote pale duniani, walipo Wazayuni na maslahi ya Marekani wasimame imara kukabiliana nao.

Msemaji wa HAMAS, Sami Abu Zuhri

 

Muhammad al Bukheiti, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Answarullah ya Yemen naye amesema kuwa, kuanzia sasa harakati hiyo itakamata meli yoyote ya Israel kama sehemu ya kuwaunga mkono na kuwasaidia wananchi wa Ghaza na wala Ansarullah haishughulishwi na makelele ya viongozi wa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wao.

Naye Brigedia Jenerali Yahya Saree, Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Yemen amesema, meli hiyo ya Israel imeshapelekwa kwenye bandari ya Yemen na katika siku za usoni pia, meli zaidi za Wazayuni zitakamatwa zitakapokuwa zinapita kwenye maji ya Yemen hadi Israel itakapokomesha jinai zake kwenye Ukanda wa Ghaza.

Kabla ya hapo pia, vikosi vya ulinzi vya Yemen vilikuwa vimetoa taarifa ambayo ndani yake vilifafanua jinsi meli hiyo ya Wazayuni ilvyokamatwa na kusema kuwa, meli zozote zinazoshirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel ni windo halali kwa jeshi la Yemen.

Tags