Muqawama waendelea kupambana kiume na Wazayuni makatili
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106040-muqawama_waendelea_kupambana_kiume_na_wazayuni_makatili
Wanamapambano wa Brigedi za Izuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la HAMAS na makundi mengine ya muqawama wa Palestina yanaendelea na mapambano yao makali na kutoa vipigo kwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliovamia Ukanda wa Ghaza.
(last modified 2023-12-15T23:23:22+00:00 )
Dec 15, 2023 23:23 UTC
  • Muqawama waendelea kupambana kiume na Wazayuni makatili

Wanamapambano wa Brigedi za Izuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la HAMAS na makundi mengine ya muqawama wa Palestina yanaendelea na mapambano yao makali na kutoa vipigo kwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliovamia Ukanda wa Ghaza.

Kituo cha upashaji habari cha Palestina limetangaza kuwa, wanamapambano wa taifa hilo wameendelea kuvitwanga kwa makombora vifaru vya Israel na kuviteketeza kwa moto katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa kituo hicho, mapambano makali zaidi ya jana Ijumaa yalishuhudiwa katika maeneo ya al Shujaia huko mashariki mwa Ghaza na Khan Yunus ambapo Wazayuni wameshtukizwa kwa mbinu za kila namna na ushujaa mkubwa wa wanamapambano wa Palestina. 

Kwa mujibu wa televisheni ya al Alam, jeshi la utawala wa Kizayuni limeendelea kukiri kuangamizwa wanajeshi wake wakiwemo wale wa kikosi maalumu cha Golan, huko kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kujeruhiwa wanajeshi wake wengine kwenye eneo hilo hilo.

Wanajeshi makatili wa Israel wakizoa majeruhi wao

 

Duru za muqawama wa Palestina zimesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unachuja mno habari kuhusu vipigo unavyopata huko Ghaza na pamoja na hayo idadi ya hasara ambayo utawala huo wenyewe unakiri kuzipata kila siku, ni kubwa. 

Abu Ubaida, msemaji wa Brigedi za al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametangaza kuwa, wanamapambano wa Palestina wameangamiza wanajeshi 36 wa Israel na kujeruhi makumi ya wengine na kuteketeza zana nyingi za kijeshi za utawala huo pandikizi na mwoga sana, katika kipindi cha saa 72 za hadi alipokuwa anatangaza habari hiyo.

Vilevile ametangaza kuwa, kambi za jangwani na vituo vikuu vya kuendeshea vita vya adui Mzayuni vimeendelea kushambuliwa na kuteketezwa na wanamapambano wa Palestina katika medani zote za vita huku wanamuqawama hao wa Palestina wakiendelea pia kuvurumisha makombora na maroketi katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwenye ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.