Mwakilishi wa Palestina UN ataka kushtakiwa Netanyahu katika mahakama ya ICC
Balozi na mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amevitaja vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni jinai ya kivita dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki na kueleza kuwa, Benjamin Netanyahu anapaswa kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya The Hague.
Riyadh Mansour, mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, utawala ghasibu wa Quds uliharibu kabisa vitongoji vya Ukanda wa Gaza na kuua maelfu ya raia.
Riyadh Mansour ameongeza kuwa, lengo la wavamizi la kutekeleza uharibifu huo wa kinyama ni kuwalazimisha Wapalestina kuhama kutoka katika makazi yao.
Kadhalika mwanadiplomasia huyo wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema, hivi sasa watoto milioni moja wa Kipalestina wanakabiliwa na hukumu ya kifo, kwa sababu wanakabiliwa na mashambulizi ya kinyama na ya upofu ya ndege za kijeshi zautawala ghasibu wa Kizayuni.
Mansour ameitaka jamii ya kimataifa kutekeleza wajibu wao wa kimaadili na kisheria ili kukomesha jinai za kutisha za utawala wa Kizayuni na kuokoa maisha ya watu wa Gaza.
Afisa huyu wa Kipalestina amesisitiza kwamba: Watoto wa Kipalestina ima wanauawa au wanakuwa mayatima na kwamba, viongozi wa Tel Aviv wanaamiliana na Wapalestina kama wanyama, vipi mtu anawezaje kuvumilia hili?
Mwakilishi na balozi huo wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amebainisha kuwa, kila mtu anataka kusitishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza, na nchi157 za dunia zimepiga kura kuunga mkono rasimu ya usitishaji vita huu, huku serikali 10 pekee ndizo zimeipinga.
Aidha ameeleza, mahhali pa Netanyahu ni katika mahakama ya ICC na siyo kuendeea kutawala Israel.