Ansarullah: Tutakabiliana na muungano wowote wa majini wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106170-ansarullah_tutakabiliana_na_muungano_wowote_wa_majini_wa_marekani
Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametahadharisha kuwa harakati hiyo itakabiliana na muungano wowote utakaoundwa na Marekani katika Bahari Nyekundu.
(last modified 2023-12-19T03:56:52+00:00 )
Dec 19, 2023 03:56 UTC
  • Ansarullah: Tutakabiliana na muungano wowote wa majini wa Marekani

Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametahadharisha kuwa harakati hiyo itakabiliana na muungano wowote utakaoundwa na Marekani katika Bahari Nyekundu.

Jeshi la Yemen hadi sasa limefanikiwa kuzishambulia meli kadhaa za Israel au zile zinazoelekea katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina baada ya mashambulizi makubwa ya kikatili ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza.

Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa, Mohammed al Bukhaiti Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameeleza kuwa  Marekani itashindwa kijeshi na kimaadili iwapo itaishambulia Yemen.   

Al Bukhaiti amesema vikosi vya ulinzi vya Yemen vina kila machuguo hatari kwa ajili ya kujibu uchokozi wowote dhidi ya nchi hiyo na kusema: Tunazishambulia meli ambazo ni mali ya Israel au zinazoelekea upande wa utawala wa Kizayuni. 

Al Bukhaiti ameashiria namna Yemen ilivyojizatiti kulinda usalama wa baharini na kueleza kuwa: Sisi tunashambulia tu maslahi ya utawala wa Kizayuni; na tutakabiliana na muungano wowote utakaoundwa na Marekani katika Bahari Nyekundu. 

Wakati huo huo Muhammad Abdulssalam Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kwa mara nyingine tena kuwa vivuko vya baharini katika Bahari Nyekundu na ya Kiarabu vipo salama na hakuna hatari yoyote kwa meli. 

Muhammad Abdulsalam