Wanajeshi 8 wa Israel waangamizwa Gaza, 44 wajeruhiwa, 10 hali mahututi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106358-wanajeshi_8_wa_israel_waangamizwa_gaza_44_wajeruhiwa_10_hali_mahututi
Neil Hagari, Msemaji wa Jeshi la utawala haramu wa Israel alitangaza jana Jumamosi kuhusu kuangamizwa askari 5 wa utawala huo na kujeruhiwa wengine 5 katika mapigano ya nchi kavu kati ya askari hao vamizi na Wanamuqawama wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Dec 24, 2023 03:27 UTC
  • Wanajeshi 8 wa Israel waangamizwa Gaza, 44 wajeruhiwa, 10 hali mahututi

Neil Hagari, Msemaji wa Jeshi la utawala haramu wa Israel alitangaza jana Jumamosi kuhusu kuangamizwa askari 5 wa utawala huo na kujeruhiwa wengine 5 katika mapigano ya nchi kavu kati ya askari hao vamizi na Wanamuqawama wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa IRNA, Hagari pia ameongeza kuwa, idadi ya askari wa Kizayuni walioangamizwa katika mashambuli ya nchi kavu huko Gaza imefika 144.

Wakakti huo huo vyombo vya habari vimeripoti kuwa katika masaa 24 yaliyopita wanajeshi wasiopungua 8 wa Isarel wameangamizwa katika mapigano yanayoendelea Ukanda wa Gaza, 44 wamejeruhiwa na kwamba 10 kati yao wako katika hali mahututi.

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo idadi ya askari jeshi wa utawala huo ghasibu walioangamizwa tokea ilipoanza operesheni ya Kimbunga cha Al aqsa hadi sasa ni 485 ambapo 158 wameangamia tangu kuanza operesheni ya nchi kavu huko Gaza.

Majeruhi wa askari vamizi

Jeshi vamizi la Israel pia limekiri kwamba askari wake 42 wamejeruhiwa katika mapigano makali kati na wanamapambano shujaa wa Kipalestina katika masaa 24 yaliyopita katika Ukanda wa Gaza.

Siku ya Jumamosi, tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya kushtukiza ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza kusini mwa Palestina dhidi ya maeneo ya utawala unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu, ili kulipiza kisasi na kufidia fedhehe ya kipigo hicho kikali cha makundi ya Muqawama, ambapo umekuwa ukiua kwa umati wakazi wa ukanda huo na vilevile kufunga vivuko vyote vinavyotumika kuingiza bidhaa na misaada ya dharura katika ukanda huo.