Jun 29, 2024 12:36 UTC
  • OIC yatahadharisha kuhusu ujenzi wa vitongoji vya walowezi unaofanywa na Israel

Katika radiamali yake kwa hatua mpya ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesema kuwa kitendo hicho cha Israel ni muendelezo wa maangamizi ya kizazi na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.

OIC imesema kuwa inapinga vikali hatua mpya za Wazayuni za kuhalalisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mipango ya kujenga maelfu ya nyumba mpya za walowezi wa Kizayuni. 

Nyumba za walowezi wa Kizayuni Ukingo wa Magharibi

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) pia imelaani kutozwa ushuru makanisa na vituo na taasisi zilizo chini ya makanisa  na milki zao huko Quds inayokaliwa kwa mabavu na pia kuendelea kupora ushuru wa Wapalestina. OIC amevitaja vitendo hivyo kuwa ni muendelezo wa  sera za Israel za kuangamiza kizazi, kuwafukuza kwa nguvu Wapalestina na kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina. 

OIC imetangaza pia kuwa, hatua na maamuzi yote yaliyochukuliwa na utawala wa Kizayuni unaoikalia Quds kwa mabavu ni kinyume cha sheria, na zina lengo la kuimarisha ukoloni katika ardhi za Palestina. OIC imesema hatua hizo za Israel ni batili kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hususan azimio nambari 2334 la mwaka 2016. 

Tags