Bagheri: Haturuhusu usalama wa kanda hii uchezewe na Israel
(last modified Wed, 07 Aug 2024 11:27:37 GMT )
Aug 07, 2024 11:27 UTC
  • Bagheri: Haturuhusu usalama wa kanda hii uchezewe na Israel

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uamuzi wa Tehran wa kutekeleza hatua hahali, madhubuti na ya kuutia adabu utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa: Iran haitaruhusu Israel ichezee usalama wa kanda hii kwa maslahi haramu ya genge la kigaidi linalotawala huko Tel Aviv.

Ali Bagheri Kani amezungumza kwa njia ya simu na Faisal al Miqdad Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria kuhusu hatua ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni ya kumuua shahidi Ismail Haniyeh Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika mji wa Tehran na kueleza kuwa: Utawala wa Kizayuni ni chanzo cha hali ya mchafukoge na ukosefu wa amani Magharibi mwa Asia kwa hatua zake za kijinai huko Yemen, Tehran na Beirut. 

Amesema, Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zinasababisha kuyumba hali ya usalama katika kanda hii kwa kuunga mkono vitendo vya kigaidi vya Israel. 

Katika mazungumzo hayo ya simu na Ali Bagheri Kani, Faisal al Miqdad Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria pia amelaani vikali kitendo cha kigaidi cha utawala wa Kizayuni cha kumuua kigaidi Ismail Haniyeh  na kusisitiza juu ya uungaji mkono wa pande zote na endelevu wa Syria kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Shahidi Ismail Haniyeh 

 

Tags