Israel yashambulia shule ya UNRWA Gaza, yaua raia 14
Raia zaidi wa Kipalestina wameuawa katika vita vya mauaji ya kimbari vya Marekani na Israel dhidi ya Gaza, huku utawala wa Tel Aviv ukiendeleza mashambulizi yake ya kikatili katika eneo lililozingirwa.
Siku ya Alhamisi, takriban watu 14 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika shambulizi la Israel dhidi ya shule inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika kambi ya wakimbizi ya Shati ambayo ilikuwa ikitumika kama makazi ya watu waliokimbia makazi yao.
Jengo hilo la makazi lililipuliwa kwa bomu katika kitongoji cha al-Daraj katika mji wa Gaza.
Israel imefanya mashambulizi kadhaa ya anga katika shule katika Ukanda wa Gaza, majengo ambapo mamia ya maelfu ya Wapalestina waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya Israel wanapata hifadhi..
Umoja wa Mataifa ulisema mwezi Septemba kwamba karibu asilimia 85 ya shule zote huko Gaza zimelengwa kwa mabomu ambapo idadi kubwa ya shule hizo zimeharbiwa kikamilifu.
Na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina lilisema asilimia 70 ya shule za UNRWA inazozisimamia zimelengwa na Israel kwa mabomu.
Utawala huo umeweka mzingiro kwenye eneo hilo, na kuzidisha hali mbaya ya kibinadamu tayari huko.
Tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari vya utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Gaza Okotoba mwaka jana, zaidi ya Wapalestina 43,400 wameuawa na zaidi ya 102,500 kujeruhiwa, wengi wakiwa ni wanawake na Watoto.