Sheikh Naim Qasim: Tutawafanya Wazayuni waombe kusitishwa vita
Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: "Maneno ya Shahidi Seyed Hassan Nasrullah ni nuru ya uongofu, na Imam Khamenei alisema kumhusu kwamba hana mithili na mfano wake.
Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu mpya wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema hayo katika hotuba aliyoitoa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya Arubaini ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah na kueleza kwamba, shahidi Nasrullah aliyaleta pamoja makundi yote ya jamii katika chama, kwa sababu Hizbollah ni chama cha watu huru, wapiganaji na watu wenye sharafu.
Amesema, sisi tunapingana vita vya kivamizi vya Israel dhidi ya Lebanon, na tunatoa salamu kwa pande za muqawama kutoka Yemen hadi Iraq na Lebanon, na kinara wao ni uungaji mkono mkubwa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH.
Amesema,vipengele vya nguvu za adui Mzayuni ni mauaji ya kimbari, mauaji ya raia, ukandamizaji, uvamizi na tabia za kishenzi.
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kwa kusema: Tutawafanya Wazayuni waombe kusitishwa vita.