Wapalestina wengine 18 wauawa shahidi Gaza
Wapalestina wengine 18 wameuawa shahidi katika jinai mpya iliyotekelezwa na jeshi la utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Duru za Palestina zinaripoti kuwa, Wapalestina hao wameuawa shahidi katika mashambulio yaliyofanywa leo na adui Mzayuni katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Gaza.
Aidha makumi ya Wapalestina wamejeruhiwa huku kukiendelea kushuhudiwa uharibifu mkubwa wa miundo mbinu katika Ukanda huo.
Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ya Ukanda wa Ghaza imetangaza kuwa, wanajeshi makatili wa Israel wameua shahidi zaidi ya raia 2,000 kaskazini mwa ukanda huo baada ya utawala huo ghasibu kuanzisha kampeni ya kuangamiza kabisa kila kitu cha eneo hilo tangu siku 40 zilizopita.
Mwezi uliopita wa Oktoba, utawala wa Kizayuni ulianzisha kampeni ya kuangamiza kabisa kila kitu ikiwa ni pamoja na wakazi wote wa kaskazini mwa Ghaza huku maelfu ya watu wakilazimika kuhama eneo hilo wakiwemo madaktari.
Hakuna chakula chochote kilichoingia kaskazini mwa Gaza tangu wakati huo huku utawala wa Kizayuni ukiendelea kuwashambulia kinyama wananchi wa Palestina ili kuwalazimisha kuhama.