Amnesty International yataka mataifa ya Ulaya yaisusie kikamilifu Israel
Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limetoa wito wa kususiwa kabisa utawala wa Kizayuni wakati huu ambapo baadhi ya mataifa ya bara Ulayaa yanachukua hatua za kuutenga utawala huo kutokana na jinai zake huko Gaza.
Amnesty International imekaribisha kwa mikono miwili uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuangalia upya uhusiano wake na utawala wa Kizayuni, ikiitaja hatua hiyo kuwa ni "ya kuchelewa lakini ni ya lazima" na kutaka kusitishwa mara moja ushirikiano wote wa kiuchumi na kijeshi na utawala huo unaoukalia kwa mabavu Palestina.
Eve Geddie Yves Geddy, Mkurugenzi wa Ofisi ya Taasisi za Ulaya katika Shirika la Amnesty International amekaribisha uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuangalia upya uhusiano wake na utawala wa Kizayuni na kusema: Mateso ya kibinadamu ya wananchi wa Palestina katika kipindi cha miezi 19 iliyopita hayaelezeki, na utawala ghasibu wa Israel bado unaendelea kufanya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza bila ya kuadhibiwa kikamilifu.
Afisa huyo ameongeza kuwa, kigugumizi na kuahirisha mambo Umoja wa Ulaya na hata uungaji mkono wa baadhi ya nchi wanachama kwa utawala unaoukalia kwa mabavu Palestina kumezifanya mamlaka za Israel kuzungumzia waziwazi malengo yao ya mauaji ya kimbari.
Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wake lazima zisitishe mara moja biashara na uwekezaji ambao unachangia katika mauaji ya halaiki na ukiukaji mwingine mkubwa wa sheria za kimataifa, Geddy alisema, akionya dhidi ya kupoteza muda ambako kunagharimu maisha ya binadamu.