Israel: Hasara inayotokana na moto unaoendelea kuwaka haijawahi kushuhudiwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i20365-israel_hasara_inayotokana_na_moto_unaoendelea_kuwaka_haijawahi_kushuhudiwa
Utawala haramu wa Israel umetangaza kuwa, moto mkubwa unaoendelea kuwaka katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, umeusababishia hasara ya mamilioni ya Dola hadi sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 28, 2016 12:16 UTC
  • Israel: Hasara inayotokana na moto unaoendelea kuwaka haijawahi kushuhudiwa

Utawala haramu wa Israel umetangaza kuwa, moto mkubwa unaoendelea kuwaka katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, umeusababishia hasara ya mamilioni ya Dola hadi sasa.

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeandika Jumatatu ya leo kwamba, serikali ya utawala huo mbali na kutakiwa kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa na kadhalika kudhamini bajeti kwa ajili ya kuzima moto huo, inatakiwa pia kuwalipa fidia watu ambao wamepata hasara kutokana na janga hilo.

Walowezi wa Kizayuni wakiwa wanakimbia kutokana na moto

Kwa mujibu wa gazeti hilo takwimu za awali zinaonyesha kwamba, hadi sasa moto huo umesababisha hasara ya baina ya Dola milioni 180 hadi milioni 900 kwa nyumba na makazi ya watu, karibu Dola milioni 500 za uharibifu wa vituo vya umeme, miundombinu na vituo vya kijamii. Aidha gazeti la Yedioth Ahronoth limekadiria kiasi cha hasara ya mamia ya mamilioni ya Dola kwa ajili ya kuuzima moto huo, suala ambalo limeutia utawala huo katika matatizo makubwa ya kiuchumi na kijamii.

Mlowezi wa Kizayuni

Limebainisha kuwa, kulipa gharama za wakulima ambao wameunguliwa mashamba yao, urekebishaji wa misitu iliyoteketea, ulipaji mishahara ya maelfu ya wafanyakazi wa idara ya zima moto na vyombo vya usalama ni mambo ambayo yanazidisha matatizo ya kiuchumi kwa utawala huo ghasibu.

Gazeti la Yedioth Ahronoth limemnukuu mmoja wa viongozi wa Wizara ya Fedha ya Israel akisema kuwa, hasara zinazotokana na moto huo ni kubwa zaidi kuliko hasara yoyote iliyowahi kuukumba utawala huo ambazo aghlabu huipata Israel kutokana na vita.