Watoto wa Kipalestina waungana kuonyesha mshikamano wao kwa mateka wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i28032-watoto_wa_kipalestina_waungana_kuonyesha_mshikamano_wao_kwa_mateka_wa_palestina
Watoto wa Kipalestina wameunda mnyororo wa kibinadamu huko katikati ya mji wa Nablos katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ili kuonyesha mshikamano wao kwa wafungwa wa Palestina waliogoma kula chakula katika jela za utawala wa Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 20, 2017 14:18 UTC
  • Watoto wa Kipalestina waungana kuonyesha mshikamano wao kwa mateka wa Palestina

Watoto wa Kipalestina wameunda mnyororo wa kibinadamu huko katikati ya mji wa Nablos katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ili kuonyesha mshikamano wao kwa wafungwa wa Palestina waliogoma kula chakula katika jela za utawala wa Kizayuni.

Wafungwa wa Kipalestina zaidi ya 1500 walianza mgomo wa kula chakula  chini ya shaari "Uhuru na Utu"  tangu Jumatatu ya tarehe 17 Aprili ambayo ilikuwa Siku ya Mateka wa Palestina kulalamikia siasa na vitendo vya kibaguzi vya utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina.  

Wafungwa wa Palestina wakiwa katika mateso ya Wazayuni 

Ripoti zinasema kuwa watoto  zaidi ya 500 na raia wengine wa Kipalestina leo Alhamisi wameelekea katika maidani ya Shuhada katika mji wa Nablos wakitokea katika ofisi ya gavana wa mji huo huku wakiwa wamebeba bendera za Palestina, picha za mateka wa Kipalestina walioko katika jela za Israel na kupiga nara za kuwapongeza na kusifu kusimama kwao kidete. Marasimu hayo yameendeshwa na makundi na mirengo mbalimbali ya Palestina katika fremu ya shughuli za kuonyesha mshikamano na kuwa pamoja na mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala ghasibu wa Kizayuni.