Iran yawapa futari mamia ya maelfu ya Wapalestina wanaozingirwa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29768-iran_yawapa_futari_mamia_ya_maelfu_ya_wapalestina_wanaozingirwa_ghaza
Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatekeleza mpango wa kuwapa futari Wapalestina karibu laki mbili katika eneo la Ukanda wa Ghaza ambalo liko chini ya mzingiro wa kinyama wa utawala haramu wa Israel.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
May 30, 2017 00:00 UTC
  • Iran yawapa futari mamia ya maelfu ya Wapalestina wanaozingirwa Ghaza

Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatekeleza mpango wa kuwapa futari Wapalestina karibu laki mbili katika eneo la Ukanda wa Ghaza ambalo liko chini ya mzingiro wa kinyama wa utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa mpango huo, kwa siku zaidi ya Wapalestina 7,500 watakuwa wakipata mlo kamili wa futari Ghaza kutoka Hilali Nyekundu ya Iran.

Mpango huu unatekelezwa katika eneo la Al Shujaiya mashariki mwa Ghaza, ambalo liliharibiwa vibaya katika hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2014.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mlo huo wa futari unasambazwa miongoni mwa watu masikini, wahitaji, familia za mashahidi, majeruhi na wafungwa Wapalestina walio katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha watu ambao nyumba zao zimebomolewa na utawala wa Kizayuni pia wanapata msaada huo. Hilali Nyekundu ya Iran imekuwa ikitekeleza mpango huo katika Ukanda wa Ghaza kwa miaka kadhaa sasa.

 

Kwa muda wa takribani miaka 10 sasa Ukanda wa Ghaza umekuwa chini ya mzingiro wa Utawala wa Kizayuni ambapo ni vigumu kufikisha bidhaa za kimsingi katika eneo hilo. Aidha utawala wa Kizayuni umetekeleza hujuma kadhaa za kinyama dhidi ya Wapalestina katika eneo hilo.