Watoto 291 Wapalestina wangali wanashikiliwa kwenye jela za utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47123
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) amesema: watoto 291 Wapalestina wangali wanashikiliwa kwenye jela za utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 30, 2018 14:24 UTC
  • Watoto 291 Wapalestina wangali wanashikiliwa kwenye jela za utawala wa Kizayuni

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) amesema: watoto 291 Wapalestina wangali wanashikiliwa kwenye jela za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hanan Ashrawi leo ametoa taarifa maalumu kwa mnasaba wa kuachiwa huru Ahed Tamimi, msichana mwanapambano wa Kipalestina na kueleza kwamba, utawala wa Kizayuni unaendelea kukiuka haki za watoto wa Kipalestina kwa kuendelea kuwaweka jela na kuwatesa watoto hao.

Katika taarifa yake hiyo, mbali na kutoa wito wa kuachiwa huru haraka wafungwa wa Kipalestina, Ashrawi amesema: utawala wa Kizayuni unakiuka haki za wafungwa wa Kipalestina na unakitumia kwa maslahi yake kimya cha duru za kimataifa ili kuendelea kuwafanyia miamala isiyo ya kibinadamu wafungwa hao.

Bi Hanan Ashrawi amebainisha kuwa Ahed Tamimi na mama yake walikamatwa na askari wa utawala wa Kizayuni na kutiwa jela kwa sababu ya kisasi cha kisiasa na akasisitiza kwamba aliyofanyiwa Ahed na raia wengine wa Palestina vimedhihirisha ukatili na ushenzi wa jeshi la utawala huo ghasibu.

Ahed Tamimi (kulia) akiwa mahakamani baada ya kutiwa nguvuni na askari wa utawala wa Kizayuni

Ahed Tamimi alikuwa kizuzini tangu tarehe 19 Disemba mwaka jana. Kosa alilokamatiwa msichana huyo wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 17, lilikuwa ni kujaribu kuwatoa askari wa Kizayuni nje ya ua wa nyumba yao. 

Hatimaye msichana huyo pamoja na mama yake Nariman waliachiliwa huru hapo jana baada ya kuwekwa jela kwa muda wa miezi minane.

Wakati huohuo Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon imetoa taarifa ya kupongeza muqawama wa vijana wa Palestina na kubainisha kwamba Ahed Tamimi, msichana wa Kipalestina, amethibitisha kuwa muqawama na kuwa ngangari katika kukabilian na uvamizi, dhulma na kiburi hakutegemei umri au jinsia ya mtu.../